Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA akikagua gwaride ndani ya Meli hiyo mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA akionyeshwa moja ya Helikopta zilizomo katika Meli hiyo mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es salaam.
………………………………………………………………………………
Meli kubwa ya Jeshi la Jamuhuri
ya China yenye Hospital ndani imewasili Leo ikiwa na Madaktari Bingwa
381,Vifaa na Madawa ya kutosha kwaajili ya kuanza kwa zoezi la Upimaji
na Matibabu Bure kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. PAUL MAKONDA ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni
Vifaa tiba vya
Kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya Upasuaji,
Vyumba vya ICU, Wodi za Wagonjwa, Vyumba vya Madaktari, Mitambo ya
kisasa, Mahabara na Sehemu ya Wagonjwa kupumzika.
Meli hiyo ya kipekee ina
Helicopter kwaajili ya wagonjwa ambapo kwa Ulimwenguni Meli za Aina hiyo
zipo Mbili pekee ambapo moja ni hii iliyokuja Tanzania na nyingine ipo
Nchini Marekani.
RC MAKONDA amesema Meli hiyo ina
mfumo maalumu wa Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China pale
inapotokea Ugonjwa umeshindikana.
Tayari Jopo la wataalamu 30
wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwaajili
ya kukarabati na kufunga vifaa vipya kwa vile vitakavyobainika
vilivyoharibika au Kufa.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.
Amewasihi Wananchi wenye magonjwa
yaliyoshindikana kwa muda mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure
chini ya Madaktari Bingwa kutoka China.
Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa
Meli hiyo Kamanda GUAN BAILIN amesema wamekuja na vifaa vya kutosha na
madaktari waliobobea hivyo wananchi Wajitokeze kwa wingi.
No comments :
Post a Comment