Ofisa Program Msaidizi wa OSIEA, Adam Antony
Mkurugenzi Mtendaji wa Mulika Tanzania, Hussein Melele.
………………………………………………………………………………………..
NA MWANDISHI WETU
JUMLA ya vijana 120 kutoka nchi
mbalimbali barani Afrika, wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la vijana
viongozi, litakalofanyika kuanzia Novemba 15 hadi 17 mwaka huu Jijini
Dar es Salaam.
Kongamano hilo lililoandaliwa na
kuratibiwa na Shirika la Open Society Initiative For Eastern
Africa(OSIEA) kwa kushirikiana na Shirika la Mulika Tanzania,
litawakutanisha vijana hao na kuweza kujadili changamoto mbalimbali
zinazowakabili ...
vijana wa bara la Afrika huku mgeni rasmi akitarajiwa
kuwa Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Waleavu, Antony
Mavunde.
Akizungumza na waandiishi wa
habari jana Jijini Dar es Salaam, Ofisa Program Msaidizi wa OSIEA, Adam
Antony, alisema kogamano hilo ni mara ya pili kufanyika baada ya lile la
mara ya kwanza kufanyika mwaka jana na kushirikisha nchi za Afrika
Mashariki pekee.
Antony alisema katika mkutano
huo,vijana hao watakaohudhuria ni pamaoja na wale ambao tayari
wameshaanzisha biashara na miradi mbalimbali huku wengi wakiwa kutoka
nchini Tanzania.
“Pia tunategemea kuwa na vijana
ambao walishawahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali zao ambao
wataweza kutoa shuhuda mbalimbali za namna walivyoweza kufanikiwa
katika kazi zao kama moja ya kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa vijana
ambao ni viongozi kwa sasa,”alisema Ofisa huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Mulika Tanzania, Hussein Melele, alisema mada
zitakazozungumziwa katika kongamano hilo ni pamoja na nafasi ya vijana
kufikia Afrika tuitakayo(Agenda 2063), vijana kushirikishwa katika ngazi
za maamuzi kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.
Jingine ni kujadili masuala ya
rasilimali zinazopatikana Afrika na namna zinavyoweza kuwasaidia vijana
katika kujiletea maendeleo kwa mmojammoja na jamii kwa ujumla.
Matarajio baada ya kufanyika kwa
kongamano hilo, Melele alisema ni kutokana na kongamano hilo
kuwakutanisha vijana viongozi na wadau wa maendeleo , mashirika ya
kitaifa, mabalozi na wanataaluma ni wazi kwamba baadaye wataweza
kuwaonesha njia ya namna gani wataweza kufanya nao kazi pamoja.
“Aidha kongamano hili litakuwa
ni daraja kwa vijana hawa kuweza kutatua changamoto katika sekta
mbalimbali hususani zinazowahusu vijana wenyewe ikiwemo za afya, ajira,
uongozi, elimu, biashara na mengineyo,”alibainisha Mkurugenzi huyo.
No comments :
Post a Comment