WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko
yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikalini.
Ametoa kauli hiyo jana jioni
(Jumanne, Novemba 7, 2017) wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la
Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema ni vema
viongozi hao kabla ya ...
kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo
halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za
wizara zao.
Pia amewataka viongozi hao
wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii
kuwa Rais Dkt. John Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao
kiutendaji.
“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha
kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza
matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka
viongozi hao wajiwekee utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za Wabunge
na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.
Pia amewataka wafanye ufuatiliaji
na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu
sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya
Serikali.
Waziri Mkuu amesema Mawaziri na
Naibu Mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo
wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.
Pia wasimamie utekelezaji wa
ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja
na ahadi alizozitoa Rais Dkt. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.
No comments :
Post a Comment