Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Ssuluhu Hassan leo ameongoza matembezi
ya hisani kwa ajili ya kusomesha Wauguzi Wakunga , matembezi hayo ya
kilometa 4.5 yalianzia kwenye viwanja vya Green Grounds, Oysterbay
jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Ssuluhu Hassan leo ameongoza matembezi
ya hisani kwa ajili ya kusomesha Wauguzi Wakunga , matembezi hayo ya
kilometa 4.5 yalianzia kwenye viwanja vya Green Grounds, Oysterbay
jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
……………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo ameshiriki
katika Matembezi ya Hisani ya Kilomita Nne na Nusu yenye lengo la
kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga.
Akihutubia mamia ya wananchi
waliojitokeza katika viwanja vya Green Ground- Oysterbay mara baada ya
matembezi hayo, Makamu wa Rais alisema takwimu za vifo vya kina mama
zimeongezeka, hivyo wazo la kusaida kuongeza idadi ya wakunga ambao
watasaidia kupunguza vifo hivyo ni zuri sana.
Makamu wa Rais alisema
“nimefarijika kusikia kuwa mwaka 2016 matembezi haya ya hisani
yalikusanya wastani wa shilingi milioni 290 pesa ambayo iliwekwa katika
fungu la kusomesha wauguzi wakunga wapya 75 katika mafunzo ya ngazi ya
cheti” . Makamu wa Rais alionesha kufurahishwa na malengo yaliyowekwa
kwa miaka miwili ijayo ya kukusanya kiasi cha shilingi milioni 300 kwa
ajili ya kusomesha wakunga wauguzi 400 katika ngazi ya cheti na diploma
kwas njia ya masafa.
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa
moja ya chanzo cha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua ni
ukosefu wa wataalam wa kuwahudumia. Takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa
zaidi ya asilimia 60 ya akina mama hawaendi kujifungua katika vituo
vyetu vya kutolea huduma kutokana na kukosekana kwa wataalam wa
kuwahudumia akina mama hao.
Makamu wa Rais aliwahakikishia
wadau wote wa sekta ya afya kwamba serikali ipo nao bega kwa bega katika
kuhakikisha wanaotaka kuwekeza katika sekta hii wanafanikisha malengo
yao. Aidha, alisema serikali inaendeleza juhudi za kuinua uchumi kwa
kuongeza idadi ya viwanda ikiwa ni pamoja na viwanda vya kutengeneza
dawa na vifaa tiba ili kuongeza upatikanaji na uboreshaji wa huduma
muhimu za afya kwa binadamu.
Makamu wa Rais aliiagiza Wizara
ya afya iusimamie kikamilifu mwongozo unaotaka kila kifo cha mama na
mtoto kinachotokana na matatizo ya uzazi kijadiliwe ndani ya saa 24
katika kituo au hospitali husika kwa lengo la kubaini chimbuko la kifo
hicho na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi
huduma zinazotolewa katika kituo husika.
Mwisho,Makamu wa Rais
aliwashukuru wadau ,wahisani na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye
matembezi hayo na kuwaomba kuendelea kushiriki na kuchangia fedha kwa
ajili ya kusomesha wakunga wauguzi.
No comments :
Post a Comment