Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiongea na watumishi wa
Wizara hiyo leo mjini Dodoma ambapo amewataka kufanyakazi kwa uadilifu
kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma. Wa kwanza kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Nicholaus William.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiongea na watumishi wa
Wizara hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi leo Mjini Dodoma.
Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma
……………
Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi amewataka watumishi wa wizara
hiyo kufanyakazi kwa uadilifu na weledi kwa kuzingatia maadili ya
Utumishi wa Umma katika kuwahudumia wananchi.
Katibu Mkuu Bi.Suzan amesema hayo
leo mjini Dodoma katika...
kikao na watumishi wa Wizara ambapo
amewahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Serikali ya
kuwatumikia wananchi kupitia sekta za wizara hiyo ambazo ni Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
“Endeleeni kuwa waadilifu na
kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, ni wajibu wa kila mmoja wetu
kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Sheria zipo ili
zitekelezwe” alisisitiza Katibu Mkuu Mlawi.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amewataka
watumishi hao kushirikiana kwa karibu na viongozi ili kuimarisha umoja
utakaoleta maarifa na ufanisi wa matokeo bora ya kiutendaji kwa manufaa
ya umma.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Bw. Nicholaus William amewaomba watumishi kuzingatia kufika ofisini
kwa muda uliopangwa na kuwahudumia wananchi ipasavyo ili kujenga taifa
lenye matokeo chanya ya kiutendaji na hivyo kuleta maendeleo katika
Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba
ya watumishi, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph
Singo amewahakikishia kuwapa ushirikiano viongozi hao kwa kufanya kazi
kwa kujituma ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Wizara.
“Tutafanyakazi kwa uadilifu kwa
mujibu wa Sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yenu kwa kufuata kasi ya
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
tukiongozwa na Sera yake ya “Hapa Kazi Tu”.
No comments :
Post a Comment