Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Tanzania Billy Mwakatage (wa nne kulia ), akipokea
msaada wa simu kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Halotel Bw. Trieu Binh (wa
tatu kushoto) katika makabidhiano yaliyofanyika Makao Makuu ya Halotel
jijini Dar es Salaam leo hii.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel
Tanzania Bw. Trieu Binh (katikati) akizungumza na Ugeni kutoka Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Tanzania ukiwakilishwa na Kamishna wa Operesheni wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage (kulia) ) katika
makabidhiano ya msaada wa simu yaliyofanyika Makao Makuu ya Halotel
jijini Dar es Salaam leo hii
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu
Mkurugenzi wa Halotel (hayupo pichani) katika makabidhiano ya msaada wa
simu yaliyofanyika Makao Makuu ya Halotel jijini Dar es Salaam leo
Naibu Mkurugenzi wa Halotel
Tanzania Bw. Trieu Binh akiteta jambo na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Billy Mwakatage, walipokutana ofisi za
Makao Makuu ya Halotel Jijini Dar es Salaam katika makabidhiano ya
msaada wa simu leo hii tarehe 02/11/2017
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Halotel Bw. Mhina Semwenda (kushoto) akielezea jambo kwa Kamishna na
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawako pichani), walipokutana
ofisi za Makao Makuu ya Halotel Jijini Dar es Salaam katika makabidhiano
ya msaada wa simu leo hii tarehe 02/11/2017
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Tanzania Billy Mwakatage akimpa mkono wa shukurani
Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Trieu Binh kwa msaada walioutoa
kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hii
Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji
……………
Kampuni ya simu za mikononi
Halotel imetoa msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili
ya kurahisisha mawasiliano ya namba ya dharura 114, katika makabidhiano
yaliyofanyika mchana wa leo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo
ambayo ilifanyika Makao Makuu ya Halotel Naibu Mkurugenzi Bw. Trieu
Binh, alisema wametoa ...
msaada huo ili kusaidia jamii kuwapata haraka
Jeshi la Zimaoto na Uokoaji kwa kutumia matandao wa halotel.
Naye Kamishna wa Operesheni wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage, ambaye amepokea msaada
huo, amesema ‘‘msaada huu utakuwa chachu kwa Jeshi na utarahisisha
mawasiliano kati yetu na jamii wakati yanapotokea majanga’’
Kamishna Mwakatage ameahidi
kuzigawa simu hizo kwenye vituo vya Zimamoto na Uokoaji hapa nchini ili
kuongeza wigo mapana wa mawasiliano haswa kwa wateja wa halotel kwani
mwanzo huduma hiyo ilikuwa haipatikani kwa kupiga 114.
Sanjari na kupokea msaada huo,
Kamishna Mwakatage aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada walioutoa na
kuwaomba waendelee kushirikiana na Jeshi hilo katika nyanja nyingine
mbalimbali ili kuboresha huduma kwa jamii
No comments :
Post a Comment