Baadhi ya vikundi vya
wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi
milioni 102 kwa ajili ya mikopo ambayo iatawasaidia katika kuendeshea
shughuli zao za biashara pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo
Mkuu wa Wilaya Kisarawe
Happiness Seneda aliyesimama akizungumza na vikundi vya wajasiriamali
kutoka kata mbali mbali katika halfa fupi ya kukabidhiwa hundi ya kiasi
cha shilingi milioni 102 kwa ajili mkopo wa kuwawezesha kiuchimi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda akizungumza jambo katika halfa fupi ya vikundi vya wajasiriamali.
Mkurugenzi mtendaji wa
halmashari ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza na vikundi vya
wajasiriamari hao hawapo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo ya
kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuwawezesha mikopo kwa ajili
ya kujikwamua kiuchumi.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
……………..
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
HALMASHAURI YA wilaya ya Kisarawe
iliyopo Mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya
tano Dk. John Pombe Magufuli kuwa na uchumi wa viwanda imetoa kiasi cha
shilingi milioni 102 kwa vikundi vya ...
wajasiriamali vipatavyo 49 vya
wakinamama,vijana pamoja na walemavu kwa lengo la kuweza kuwasaidia
kuendesha shughuli zao mbali mbali za biashara mbali mbali ikiwemo na
kuwawezeha ili waweze kujikita zaidi katika kujenga viwanda vidogo
vidogo.
Akizungumza katika halfa fupi ya
kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyohuduriwa na viongozi mbali mbali wa
serikali pamoja na viongozi wa vikundi hivyo Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama alisema kwamba fedha hizo
za mikopo zimetolewa kwa vikundi hivyo kutokea kata zote 17 ambapo
zimetokana na makusanyo ya mapato ya ndani.
Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa
kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuweza kukuza uchumi
wa nchi kutokana na kuweza kuwapa fursa wajarisiamali hao kupania
wigo wa kibiashara pamoja na kuanzissha viwanda vingine vidogo vidogo
ambayo vitaweza kuongeza upatikanaji wa ajira mpya na kupunguza wimbi la
umasikini.
“Kwa kweli sisi kama halmashauri
ya Wilaya ya Kisarawe tumejipanga kuweka mipango madhubuti katika
kuviwezesha vikundi vyetu vya ujasiriamali kwa kutumia fedha zetu ambazo
zinatokana na makusanyo ya mapato ya nadani, hivyo vikundi hiivi ni
moja ya mipango yetu katika kuhakikisha ile asilimia 10 iliyotengwa
inawafikia walengwa na kuweza kuleta mabadiliko chanya ya
kimaendeleo,”alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe Happiness Seneda ameviasa vikundi vyote vilivyopata mkopo huo
hususan kwa wakinamama kuachana kabisa na vitendo vya kutumia fedha
hizo vibaya kwa shughuli ambazo hazina manufaa yoyote kwa jamii, kama
vile kuwachezesha watoto wao ngoma wakati wa kufunga shule pamoja na
kununulia madela kitu ambacho amekilaani vikali.
Aidha Seneda alisema kuwa malengo
ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha wananchi wake wanawezeshwa
kwa namna mbali mbali ikiwemo kuwapatia mikopo ambayo itaweza kuwapa
fursa ya kukuza biashara zao pamoja na wengine kufanya biashara zao
ndondogo amabzo zitaweza kuwapatia kipato na kujikwamua kiuchumi.
“Jamani mimi kama kiongozi wenu
napenda kuwaasa wale wote mlionufaika na mkopo huu, kuhakikisha
mnazitumia vizuri fedha hizi hasa kwa upande wa wakinamama ambao
wamekuwa na tabia pindi wanapotata pesa wanazitumia katika matumizi
mengine ya kununulia madela kwa ajili ya sare pamoja shughuli nyingine
kama vile kuwacheza ngoma watoto wao hii tabia kwa kweli sipendi kuiona
katika Wilaya yangu,”alisema Seneda.
Nao baadhi ya wajasiriamali ambao
wamenufaika na mkopo wa fedha hizo akiwemo Monica Muhoza ambaye ni
mlemavu wa miguu, Faudhia Kasikasi, pamoja na Gudluck Akyoo
wameshukuru uongozi mzima wa halmashauri ya Kisarawe na kusema kuwa
fedha hizo walizopatiwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao kwani
zitaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi pamoja na kujikimu kimaisha na
kuendesha familia zao.
VIKUNDI hivyo vya wajasiriamali 49
kutoka kata 17 za Wilayani Kisarawe zimewahusiha wakinamama, vijana,
pamoja na makundi vya walemavu ambapo vimepata mkopo wa fedha hizo kiasi
cha shilingi milioni 102 ikiwa ni makusanyo ya mapato ya fedha za
ndani.
No comments :
Post a Comment