Mkurugenzi
Mkuu wa GEPF Daud Msangi, sheria
ya mfuko inatamka wazi ya kuwa mwanachama anaweza kutumia sehemu ya
mafao yake kama dhamana ya kupata mkopo wa nyumba ya makazi.
Na
CHRITIAN GAYA
Kutokana na upeo wa michango au
mafao ya pensheni, umilikaji wa nyumba ni sehemu ya upangaji mzuri wa jinsi ya
kustaafu. Kumiliki nyumba wakati wa kustaafu inawalinda wastaafu kutokana na
mahitaji ya mtiririko wa fedha mkononi. Pamoja na hayo tena inawalinda ...
wastaafu
kutokana na maamuzi mabaya ya uwekezaji, na faida mbaya inayotokana na
uwekezaji ikiwemo na mfumuko wa bei ambao hauendi na ukali wa maisha wa wakati
huo.
Nyumba inamwandaa mstaafu na maisha
yenye heshima usoni mwa jamii na yenye utu mzuri wa hali ya maisha. Umilikaji
wa nyumbani kwa kweli huchangia kiasi kikubwa kwa wastaafu kwa ajili ya
kuwaandaa maisha ya ulimwengu wa kustaafu na katika kuwatengenezea staili ya
miaka yao ya mwanzoni kabla hawajastaafu.
Singapore wanachama wa mfuko wa hifadhi
ya jamii wanaruhusiwa kutumia asilimia 75 ya akiba yao ya michango ya pensheni
kwa ajili kukopeshewa nyumba au kwa ajili ya kununulia nyumba maalumu
anayohitaji.
Nyumba ni rasilimali ambayo
inawezekana kubadilishana na kitu chochote. Kwa sababu thamani ya nyumba
inatambulika. Kijamii nyumba inachangia kuhamasisha na kuboresha nafsi ya mtu,
utu, usalama na kutambuliwa mbele za watu. Kisiasa, nyumba bora inapunguza
vitishia vya kisiasa vinavyotokana na kugandamizwa na kuchanganyikiwa hasa kwa
watu wanaoishi kwa mazingira hatarishi na makazi yasiyokuwa rasmi
Wakati Mauritius na Afrika Kusini mifuko ya hifadhi za jamii
yanaruhusu kutoa mikopo moja kwa moja kwa wanachama na hata vilevile wanachama
kutumia sehemu ya theruthi mbili ya mafao yao ya baadaye kama amana ya kumpatia
mikopo benki na kupata mkopo wa nyumba kutoka taasisi za nyumba au mashirika ya
nyumba ya nchi hizo kama vile Shirika la Nyumba la Taifa.
Mafao yaliyosalia yanaachwa kama
yalivyo bila kuguswa mpaka wanachama atakapofikia wakati wa kustaafu kwa hiari
au kwa lazima. Wanachama waliokopa wanalipa riba kwa muda wote na kuhurusiwa
kuingilia mafao kulipa deni halisi alilokopa wakati utakapofika muda wake wa
kawaida wa kustaafu. Kwa Afrika kusini viongozi wa hifadhi ya jamii
wanapandisha mkopo wa nyumba kwa kutumia soko la mtaji kwa kutoa amana ya
pensheni ili kumwezesha mwanachama kumiliki nyumba
Katika kutambua umuhimu wa ungezeko
wa uzalishaji nyumba kwa ajili ya kuhudumia watu wanaongezeka kila siku, mkurugenzi mkuu wa
GEPF, Daud Msangi anasema serikali
mara kwa mara imekuwa ikiaangalia
uwezekano wa kuwa na ufumbuzi wa aina
mbalimbali na hata vilevile kushawishi ushiriki wa sekta za watu binafsi ili
kufikia lengo hili la nyumba. Uwezekano wa kupata mikopo ya fedha kwa
waendelezaji na wanunuzi kumekuwa ni mojawapo ya sababu zilizochangia kuwa na
uhaba wa nyumba.
Anasema
Sheria ya Mfuko wa mafao ya kustaafu GEPF ya mwaka 2013 inayoanzishwa kwa manufaa ya waajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi ikijumuisha watu waliojiari
wenyewe, inatoa amana ya mkopo
wa nyumba ya makazi katika kutambua umuhimu wa jambo hili kwa wastaafu wake.
"Inatamka
wazi ya kuwa mwanachama wa Mfuko wa GEPF anaweza kutumia sehemu ya mafao yake
kama dhamana ya kupata mkopo wa nyumba ya makazi kulingana na utaratibu
ulioelekezwa na mamlaka. Na kuonesha ya kuwa sheria hiyo inakwenda na wakati
hasa kwa kuwajali wateja wake inasema wazi ya kuwa mwanachama anaweza kwa
ruhusa ya bodi kuchukua sehemu ya michango yake kwa namna na kwa kiasi
kitakachokuwa kimeainishwa kwenye Kanuni," Msangi anafafanua zaidi.
Anasema kulingana
na Sheria ya GEPF ya mwaka 2013 amana ya
mwanachama” maana yake ni michango ya mwajiriwa, michango ya mwajiri na riba
yake ambayo ipo kwenye akaunti ya mwanachama.
Sheria hiyo inaruhusu wanachama wake
kuingilia michango yao ya akiba ya pensheni kwa ajili ya amana ya kujipatia
nyumba ya mkopo.
"Mkopo huu ni kwa
ajili ya kujenga nyumba ya mwanachama wa GEPF na hutolewa kwa mwanachama
aliyefikisha umri wa miaka 55 ambaye amechangia kwa muda usiopungua miezi 180,"
Msangi anakumbusha zaidi.
Mwandishi
wa makala hii ni mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni, mshauri na mtaalamu wa
masuala ya pensheni. Kwa maelezo zaidi gayagmc@yahoo.com unaweza kutembelea tovuti hakipensheni monitor online na hakipensheni blog Simu
+255 655 13 13 41
No comments :
Post a Comment