Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akikabidhi
moja ya kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 wanaoishi kwenye mazingira
magumu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina
ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
na BancABC Tanzania.
Baadhi wa watoto wanufaika na kadi za bima wakiwa na walezi wao
wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Wazee Ummy Mwalimu
Baadhi ya wafanyakazi wa Kitengo cha magonjwa ya dharura kutoka
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifuatilia kwa umakini hotuba ya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati
wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao ni
mayatima
Baadhi ya wafanyakazi BancABC Tanzania wakifuatilia kwa umakini hotuba
ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu
wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao
ni mayatima.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akiongea na
Mkurugenzi wa Kitego cha wateja wakubwa na wadogo wa BancABC Joyce Malai
wakati wa kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha
magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC
Tanzania.

Picha ya Pamoja
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu aikisisita
jambo kwa Mkurugenzi wa Kitego cha wateja wakubwa na wadogo wa BancABC
Joyce Malai wakati wa kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya
Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
BancABC Tanzania.
BancABC,
ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imeshirikiana na Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ili kutoa huduma ya bima ya afya itakayofaidisha watoto 100
ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia mradi mpya
wa afya wa Muhimbili uliozinduliwa leo.
Akizindua
mpango huo wa Afya wa Muhimbili Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliishukuru BancABC kwa
kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili katika suala hilo la kutoa huduma
ya bima ya afya kwa watoto.
Alisema
mradi huo wa Muhimbili kushirikiana na BancABC unaendea sambamba kabisa
na malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa jamii
inapata huduma ya Afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
kwani watoto ndio moja ya makundi ambayo huathirika sana wasipopatiwa
huduma za Afya za uhakika.
“Natoa
wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa na BancABC kwa
ushirikiano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafungulia watoto
wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa
uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha tasilimu pale mtoto
anapougua,” alisema.
Alitoa
wito pia kwa watoa huduma za kifedha nchini pamoja na mashirika mengine
kuhakikisha yanaiga mfano huo wa BancABC kwani wizara yake iko
tayarikushirikiana na taasisi ambazo ziko tayari kuimaisha huduma katika
sekta ya afya hasa upande wa utoaji huduma.
Naye
Mkuu wa Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa
kati, Bi Joyce Malai alisema BancABC inatambua umuhimu wa kuwa kampuni
inayowajibika katika masuala ya kijamii kwa kurudisha kwa jamii sehemu
ya faida na hasa katika sekta muhimu sana ya afya, dhamira hii ya
BancABC kusaidia kwenye kuwezesha Afya ya watoto ni yamsingi sana kwa
kuwa pia inasaidia serikali kufikia malengo yake.
Alisema
baada ya kufungua akaunti hizo, wazazi wa watoto wenye akaunti hizo
watakuwa wanahimizwa wakewe hela mara kwa mara kwa ajili ya bima ya
watoto wao ili wapate huduma kupitia akaunti hizo za Mwangaza Junio Kids
Accountambayo haina tozo ya kila mwezi.
Bi
Joyce Malai aliongeza kuwa huduma hiyo ya bima haitakuwa na masharti
kuhusu umri. “Wazazi wanaweza kufungua akaunti kwa mtoto zaidi ya moja
na kuweka fedha kiasi chochote wanachotaka kwani itasaidia kuhakikisha
watoto wao wana bima,”.
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa, Prof. Lawrence Museru,
aliishukuru BancABC kwa ushirikiano huo na kusema hatua hii haitasaidia
watoto kupata tu huduma za afya kwa kupitia bima, bali itawajengea pia
utamaduni wa kuweka akiba katika benki kuanzia utotoni hadi wanapokuwa
watu wazima ili wapange mambo yao vizuri .
“Kwa
sasa akaunti hizi zitafunguliwa na wazazi wao ila watakuwa wakitambua
umuhimu wa huduma hii na wataendelea nayo hadi ukubwani,”alisema na
kutoa rai kwa wazazi watumie fursa hiyo vizuri.
No comments :
Post a Comment