Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutiliana
saini makubaliano ya Dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi
bilioni 80.4) kwa shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo kupitia
mashirika ya Umoja wa mataifa kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye
ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Balozi wa Uswidi
nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt.
Kwa msaada huu,
tunawezesha uchukuaji hatua unaoendana na sera ya nje inayozingatia haki
za wanawake ya Uswidi na pia jitihada zinazolenga, miongoni mwa mambo
mengine, ajira yenye hadhi na haki za watoto. Hii inadhihirisha
mwendelezo wa uhusiano wa karibu na Umoja wa Mataifa na serikali ya
Tanzania wenye lengo la kuleta maendeleo yenye usawa na jumuishi zaidi,”
alisema Balozi.
Akisisitiza utayari wa kuendelea kuisaidia
Tanzania na Umoja wa Mataifa, Balozi alitumia fursa hiyo kuthibitisha
kuyapokea kwa moyo mmoja mageuzi ya Mfumo wa UN chini ya Mpango wa
Kufanya Kazi Pamoja na kutambua njia fungamanifu zinazotumika na thamani
inayopatikana kutokana na mchango wa mashirika ya UN katika lengo moja
kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania, washirika wa kijamii na vyama
vya kiraia.
Balozi
wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla hiyo fupi ya kutiliana
saini makubaliano ya ya Dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi
bilioni 80.4) kwa shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo
kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Akizungumza baada
ya kutiliana saini makubaliano, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Rodriguez alitoa shukrani kwa serikali na
watu wa Uswidi kwa msaada wao endelevu akiipongeza Uswidi kwa kuwa
mshirika wa maendeleo asiyeyumba katika shughuli za Umoja wa Mataifa
Moja na pia kwa Tanzania.
“Uswidi imekuwa mshirika wa kuaminika
wa Tanzania na Umoja wa Mataifa kwa miongo mingi. Kwa kulenga wale walio
wanyonge kabisa katika jamii hii, rasilimali hii itatoa mchango muhimu
sana katika kushughulikia mahitaji ya wale ‘walio chini sana’ kama
inavyoelekezwa katika Malengo ya Ulimwengu,” alisema.“Mchango huu
utauwezesha Umoja wa Mataifa kuweza kufanya kazi katika masuala mapana
mengi kama vile kuhamasisha fursa za ajira zenye hadhi kwa Watanzania
maskini, kuendeleza kanuni za utawala bora, na nafasi ya uongozi wa
wanawake katika masuala ya siasa na vilevile kuzuia vitendo vya ukatili
dhidi ya wanawake na watoto,” aliongeza.
Mtaalam
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akikabidhi hati
za makubaliano kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi
wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh.
Katarina Rangnitt wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya
dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4)
zilizotolewa na Serikali ya Uswidi kwa ajili ya shughuli za maendeleo
katika miaka minne ijayo kupita mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Balozi
wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt na Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez (kulia)
wakitiliana saini makubaliano ya dola za Marekani milioni 36 (takribani
Shilingi bilioni 80.4) kwa shughuli za maendeleo katika miaka minne
ijayo kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Uswidi jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi
wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh.
Katarina Rangnitt wakibadilishana hati za akubaliano ya Dola za Marekani
milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4) zilizotolewa na Serikali
ya Uswidi kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo
kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment