Dk.Fatma
Kiango kutoka hospitali ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam akitoa
mada kuhusiana na ugonjwa wa Saratani ya matiti kwa baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya TDL.
Dk. Joseph
Matemba kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la JHPIEGO- Mbeya
akitoa mada ya Saratani ya matiti kwa wafanyakazi wa kiwanda cha
TBL-Mbeya
Dk. Fridolin
Mujuni kutoka hospitali ya Bugando jijini Mwanza akitoa mada kuhusiana
na ugonjwa wa Saratani ya matiti kwa baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda
cha TBL cha Mwanza.
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TBL cha Ilala wakimsikiliza Dk.Namwai
Makame alipokuwa akiwapatia maelezo kuhusiana na Saratani ya matiti
wakati wa zoezi la kuwapima wafanyakazi wa kampuni hiyo lililofanyika
kiwandani hapo.
………………………………………………………………
-Yaendesha zoezi la kupima afya za wafanyakazi
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL
Group katika viwanda vyote nchini mwishoni mwa wiki walipimwa Saratani
ya matiti ikiwemo kupatiwa elimu juu ya ugonjwa huu ambao umekuwa
ukiongezeka kwa kasi nchini.
Meneja Mawasiliano wa Mawasiliano wa kampuni
hiyo,Zena Tenga,amesema kuwa zoezi hili limetekelezwa nchini ya Mpango
wa kuimarisha afya za... wafanyakazi pamoja na familia zao unaojulikana
kama ‘Afya Kwanza’ ikiwa pia ni kuadhimisha mwezi wa Saratani ya matiti
duniani kwa vitendo.
Tenga amesema tangu mpango huu uanze kutekelezwa na kampuni umeanza kuonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa wafanyakazi wanapata fursa ya kupata elimu ya afya ya kujikinga na magonjwa mbalimbali elimu ambayo pia inatolewa wa familia za wafanyakazi.
“Mwitikio
wa wafanyakazi wetu wote kushiriki katika programu hii ni mzuri kama
ambavyo wengi wamejitokeza kupimwa na kupatiwa ushauri wa jinsi ya
kuepuka ugonjwa wa Saratani ya Matiti na kujua dalili za ugonjwa huu
mapema pindi unapojitokeza ili kuwahi kufanyiwa uchunguzi na kupata
matibabu”.Alisema Tenga.
Alisema
mbali na kampuni kuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha wafanyakazi
wake na familia zao wana bima ya afya na kuwa na zahanati katika viwanda
vyake bado imeonelea kuna umuhimu wa kuhakikisha wanapata elimu ya
kinga kwa kuwa kinga ni bora kuliko matibabu na kuongeza kuwa mbali na
wafanyakazi kupatiwa elimu na ushauri nasaha kuhusiana na magonjwa
mbalimbali pia wanapata fursa ya kushiriki kufanya mazoezi ya pamoja
yanayoshirikisha pia familia zao pia wamekuwa wakipatiwa elimu kuhusiana
na masuala ya umuhimu wa lishe bora.
“Changamoto ya ongezeko la magonjwa nchini
inachangiwa na sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni mitindo ya maisha ya
kisasa na ukosefu wa elimu ya lishe bora,kupitia jukwaa hili la
Afya kwanza wengi wanaelimika na kujua umuhimu wa mazoezi,lishe bora na
mtu mwenye afya njema anatakiwa awe katika hali gani”.Alisema Tenga.
Tenga alisema katika kufanikisha zoezi hili la
kupima Saratani ya Matiti kampuni imetumia wataalamu wa afya kutoka
hospitali mbali kama ambavyo imekuwa ikifanya katika utekelezaji wa
Programu ya Afya Kwanza.
Mmoja
wa madaktari walioendesha zoezi la kupima Saratani kwa wafanyakazi na
familia zao jijini Dar es alaam,Dk.Fatma Kiango kutoka hospitali ya
wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,amesema kuwa Tanzania ni moja ya
nchi ambazo zimekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani kwa kasi
hususani katika miaka ya karibuni mojawapo ikiwa ni saratani ya Matiti
ambayo inaendelea kuathiri wanawake wengi.
Alibainisha baadhi ya sababu za ugonjwa wa saratani ya matiti kuwa ni historia ya saratani katika familia,
mfumo wa kazi unaoweza kusababisha kansa ,mfumo wa maisha kama vile
uvutaji wa sigara, mfumo wa kula. “Ni muhimu kutafuta matibabu ya
haraka, ukiona dalili zozote za saratani ya matiti, usisubiri mpaka uwe
katika hali mbaya ndio uende hospitali, kwa sababu baada ya kuchunguzwa
mapema unaweza kutibiwa kwa ufanisi,” alisema Dk. Kiango.
No comments :
Post a Comment