Tuesday, October 31, 2017

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AZITAKA TAASISI ZA FEDHA KUPUNGUZA RIBA YA MIKOPO

MAKAMU wa Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN, amezinduzi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, tukio litakalofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoa huduma ndogo za fedha kupunguza riba za mikopo na tozo mbalimbali ili kufanikisha lengo la Sera hiyo ambalo ni kuimarisha huduma jumuishi za fedha kwa kujenga mazingira wezeshi yatakayoleta ufanisi wa utoaji wa huduma ndogo za fedha nchini kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Ninawaomba pia muongeze ubunifu katika kutoa huduma zinazohitajika na wananchi wa kipato cha chini pamoja na kupeleka huduma hizo katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao au biashara zao” aliongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan

Alizitaka taasisi za huduma za fedha kuwaelimisha wananchi kabla ya kutoa huduma hizo ili kupunguza athari wanazozipata wananchi.

Ni matarajio yangu kuwa, Wizara ya Fedha na Mipango itashirikiana na wadau katika kutekeleza Sera hii na kuhakikisha malengo ya Sera ambayo ni kukuza uchumi na kupunguza umaskini yanafikiwa” alisisitiza

No comments :

Post a Comment