Wataalam
kutoka , Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ua Udhibiti wa
Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo
yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani (hayupo pichani).
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda,
Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia
ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.
Medard Kalemani (hayupo pichani)
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande akifafanua jambo katika kikao hicho.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya hati
na Madini, Asteria Muhozya (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, Salum Mnuna katika
kikao hicho
…………………
Asteria Muhozya na Greyson Mwase.
Timu
ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya
kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa ...
mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani Singida.
mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani Singida.
Kabla
ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017
wamefanya kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam
kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli
za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
Akizungumza
katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema maandalizi hayo ni juhudi
za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za
kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta
manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la
Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika
Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5
Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa
Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti
wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na Eyasi nchini Tanzania.
Dkt.
Kalemani amesema baada ya Rais wa Uganda kukubali ombi hilo yalianza
maandalizi kupitia vikao mbalimbali ambapo hatua iliyofikiwa kwa sasa ni
wataalam kukutana na kubadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa shughuli
za utafiti katika maziwa husika.
Amesema
wataalam wataanza kwa kufanya ziara ya siku mbili katika Ziwa Eyasi
Wembere mkoani Singida ili kupata picha halisi kabla ya kuanza kwa
majadiliano ya kubadilishana mawazo ya namna bora ya utafiti katika
maziwa husika.
“
Sisi kama Tanzania tupo tayari kubadilishana uzoefu na wataalam wa
Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja; hata hivyo
pia tupo tayari kubadilishana nao uzoefu kwenye masuala ya gesi kwa
kuwa tuna utaalam huo, lengo likiwa ni kuimarisha sekta hizi za mafuta
na gesi kwa nchi zote mbili,” amesema Dkt. Kalemani.
Ameongeza
kuwa kwa kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia,
wapo tayari kutuma wataalam nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti
wa gesi nchini Uganda.
Kwa
upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya
Madini Nchini Uganda na kiongozi wa ujumbe huo, Robert Kasande amesema
kuwa wapo tayari kubalishana uzoefu ambapo watalenga katika kuangalia
tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka
mikakati ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa
kushirikiana na Tanzania.
No comments :
Post a Comment