Meneja wa Kituo cha kulea watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Nitetee Foundation,
Johansen Emmanuel akipima shinikizo la dmu kabla ya kutolewa damu katika
uchangiaji damu wa hiari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ashura jijini
Mwanza jana
Mkurugenzi wa Chuo cha Urembo cha
NIFO Beauty College cha jijini Mwanza Flora Lauwo katikakati akichangia
damu katika maadhimisho ya Siku ya Ashura.Kulia ni Zawadi Mihayo na
kushoto ni Hadija Hussein ambao ni wanafunzi wa chuo hicho.Jumla ya
chupa 445 zilikusanywa jana.
Wanafunzi wa Chuo cha Urembo cha
NIFO Beauty College cha jijini Mwanza Happyness Corneli kulia na Hadija
Hussein wakitoa damu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ashura
yaliyofanyika jana ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein (A.S)
na mwanzo wa mwaka wa Kiislamu.
Maulana
Sheikh Seyyid Abass Bakriy (kulia) akitolewa damu katika maadhimisho ya
Siku ya Ashura yaliyofanyika jijini Mwanza jana kwa jamii na waumini wa
dini ya Kiislamu kuchangia damu kwa hiari.Kushoto ni Sulemani Mpuhu.
…………………………………………………………………….
Na Baltazar Mashaka, Mwanza
Taasisi
za The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania na The Bilal Muslim
Mission of Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Damu Salama Kanda ya
Ziwa zimekusanya chupa 445 za damu.
Zoezi
hilo la kuchagia damu kwa ...
.hiari ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ashura kuashiria kuanza kwa mwaka wa Kiislamu lakini pia ni kumbukumbu ya kuuawa kwa Imam aliyeuawa huko katika Jangwa la Karbala nchini Iraq.
.hiari ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ashura kuashiria kuanza kwa mwaka wa Kiislamu lakini pia ni kumbukumbu ya kuuawa kwa Imam aliyeuawa huko katika Jangwa la Karbala nchini Iraq.
Mwenyekiti
wa The Desk & Chair Foundation Alhaji Sibtain Meghjee ambaye pia ni
mwenyeiti wa Bilal Muslim alisema jamii inatakiwa kubadili mitizamo
hasi na kuona umuhimu wa kujitolea kwa hiari kuchangia damu kuwa ni
jambo la kheri ili kuokoa maisha ya watu wengine na itumie sikukuu kubwa
za Pasaka, Krismasi na nyingine, zikiwemo sherehe za arusi kuchangia
damu.
“Kuchangia
damu kutasaidia kupunguza vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu.Watu
wajitolee iwe ni wakati wa huzuni na furaha,wazitumie siku kuu kubwa
kuchangia damu na kufanya hivyo watakuwa wamefanya jambo jema na urithi
wa kukumbukwa na jamii,”alisema.
Alhaji
Meghjee alieleza kushangazwa na baadhi ya watu kuhoji kuwa
wanapochangia damu wananufaika na nini ilhali wakifahamu damu haina
kiwanda, haizalishwi popote zaidi ya binadamu mwenyewe na hivyo wanaunga
mkono agizo la Wazitri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto la kuchangia damu kwa hiari.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi wa Chuo cha Urembo cha NIFO Beauty College Flora
Lauwo alisema kuwa amefanya kazi nyingi za jamii na kubaini watu wengi
hawataki kuchangia damu kutokana na hofu ya afya zao kutokana na kukosa elimu ya kustosha.
Alishauri
kutokana na watu wengi kupoteza maisha sababu ya ukosefu wa damu
serikali kutunga sheria ili kila mtu mwenye afya njema achangie damu
licha ya kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa elimu kwenye jamii yenyewe
kutokuona jambo hilo ni muhimu .
Katika
zoezi hilo Lauwo alikuwa miongoni mwa wachangiaji wa damu, wakiwemo
wanafunzi 50 wa chuo hicho cha urembo cha NIFO Beauty na kwamba
wameguswa na zoezi hilo kutokana na mtoto mmoja aliyetajwa kwa jina moja
la Musa anayesumbuliwa na tatizo la saratani ya damu na hivyo kuhitaji
kuongezewa kila mara.
Aidha,
Kiongozi wa Shia Khoja Ithna Asheri Mwanza Maulana Sheikh Seyyid Amiri
Abass Bakriy alishauri Watanzania bila kujali imani zao za dini wala
makabila yao kujitoa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watoto,
wajawazito na watu maradhi mengine kwa sababu ukichangia damu ili kuokoa
mtu mmoja utakuwa umeokoa maisha ya watu wengi.
“Ukijitolea
kwa Siku hii ya kumbukumbu ya Imam Hussein utapata thawabu zaidi na
unavyodhani.Hivyo Watanzania msiogope kuchangia damu kwa kuwa ni muda
mfupi tu wa kujitolea damu hiyo na inarudi kwa kasi,”alisema.
Maulana
Bakriy aliongeza kuwa katika maadhimisho hayo ya Siku ya Ashura ni
mfano wa kuigwa na wapenda haki, ukweli, heshima, uadilifu na usawa
kwenye jamii zetu katika kuondoa dhuluma, unafiki na ujinga kwa kuwatia
moyo waumini na wanyonge wanaokandamizwa.
No comments :
Post a Comment