Monday, September 4, 2017

MTAALAMU KUTOKA JAPAN ATEMBELEA TBL NA KUKIRI TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA

japan tbl 10
Profesa Umanda, ambaye aliongozana na Afisa wa fedha  wa  shirikisho la wenye viwanda Tanzania,(CTI) Anna Kimaro  ambaye kwa sasa anasoma katika chuo hicho,  amesema  uwekezaji wa sekta ya viwanda ni moja ya njia ya kukuza uchumi wa nchi kinachotakiwa kufanyika ni kuwa na viwanda vyenye nyenzo za teknolojia ya kisasa na wataalamu ambavyo vinaweza kuzalisha bidhaa bora zinazoweza kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
 
Alisema kuwa amefurahi kuona nchini Tanzania kuna kiwanda kikubwa kama TBL ambacho kinafanya uzalishaji kwa kutumia mifumo na teknolojia za kisasa sambamba na viwanda vilivyopo katika nchi zilizoendelea na kuongeza kuwa uwekezaji katika sekta ya viwanda ukifanyika kwa umakini utawezesha sera ya Tanzania kuelekea katika nchi ya viwanda kufanikiwa kwa haraka.
 
Akiongea  na ujumbe huo,Afisa Mawasiliano wa TBL Group,Abigail Mutaboyerwa alieleza  jinsi kampuni ya TBL Group mbali na kufanya uzalishaji kwa kutumia  mifumo na teknolojia za kisasa katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Arusha,Mbeya na Dar es Salaam inatekeleza sera  ya ‘Dunia Maridhawa’ (Better world) ambayo imelenga kukuza viwanda  sambamba na kuboresha shughuli za utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na kuboresha maisha ya watu kwenye jamii ambapo kampuni imewekeza.
“Sera ya Dunia Maridhawa malengo yake yanashabihiana na malengo endelevu ya Milenia ya Umoja wa mataifa (SDG’s) na sisi kama kampuni tunahakikisha tunafanikisha  malengo haya na kwa kiasi kikubwa tumepata mafanikio hususani katika maeneo ya kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira,matumizi mazuri ya maji ,kuendesha kampeni za utunzaji wa vyanzo vya maji,matumizi ya nishati mbadala zisizo na athari kwa mazingira,kuharibu taka kwa kutumia teknolojia za kisasa, na utakatishaji wa maji taka”.
 
Mutaboyerwa alisema katika kuhakikisha viwanda vya kampuni vinafanya uzalishaji bila  athari  kwa mazingira kampuni imeanza kutumia teknolojia mbadala zisizochafua  hewa katika mchakato wa uzalishaji  ambapo katika kiwanda cha  TBL Mwanza  kinafanya uzalishajinkwa kutumia pumba za mchele na katika kiwanda cha  TBL Mbeya   kimefunga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua ambao utatumika katika shughuli za uzalishaji.
 
Aliongeza kusema kuwa matarajio ya matumizi ya teknolojia mbadala za kuzalisha nishati ya umeme ni kupunguza tani 130 za hewa chafu (Carbon Emmision) kwa mwaka na kampuni inao mkakati kuhakikisha teknolojia hii inasambazwa katika viwanda vyake vyote  vilivyopo nchini  na aliongeza kuwa kampuni yetu imefanikiwa kupunguza matumizi ya maji   kutoka hectolita 6 ilizokuwa inatumia miaka ya karibuni hadi hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa.
 
Mbali na mazingira alieleza mkakati wa kampuni wa kufanya kazi na wakulima ambao wanaiuzia malighafi ambao umeanza kuleta mafanikio kwa kuwanufaisha wakulima wa Shahiri wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro sambamba na wakulima wa zabibu mkoani Dodoma. “Kupitia mpango wetu wa kuwezesha wakulima maisha yao yamebadilika kuwa bora na kupanua wigo wa ajira mashambani na tumejipanga kufanya kazi  na wakulima wengi zaidi nchini  lengo letu kubwa likiwa ni  kuinua maisha yao,kuongeza kasi ya kukua uchumi na kujenga mfumo mzuri na endelevu wa  kupata malighafi kwa ajili ya viwanda kampuni ya TBL Group kwa hapa nchini”.Alisisitiza.
 
Alimalizia kwa kusema kuwa TBL Group chini ya kampuni mama ya ABINBEV itahakikisha  inashirikiana na serikali kufanikisha mkakati wa kujenga Tanzania ya viwanda na iko tayari  kubadilishana uzoefu na taasisi mbalimbali za  hapa nchini na nje ya  nchi “Tunaamini tukishirikiana tutafanikiwa,ndio maana tumefungua  milango kwa wageni kutoka taasisi mbalimbali ambao wamekuwa wakija kutembelea viwanda vyetu kwa ajili ya kujifunza mambo  mbalimbali”Alisisitiza
1.Profesa Umanda kutoka Japan (kulia ) akibadilishana mawazo na Afisa Mawasiliano wa TBL,Abigail Mutaboyerwa (katikati) na Anna Kimaro kutoka CTI kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda
Japan tbl tour 1
Profesa Umanda kutoka Japan (kulia ) akibadilishana mawazo na Afisa Mawasiliano wa TBL,Abigail Mutaboyerwa (katikati) na Anna Kimaro kutoka CTI kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda
japan tbl 5
Profesa Umanda akipata maelezo kutoka kwa Mtalaam wa upishi wa bia wa TBL Group Christian Tarimo alipofanya  ziara ya mafunzo kiwandani hapo
japan tbl 6 japan tbl 9 
Mtaalamu wa  masuala ya sera na uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Yamoguchi kilichopo nchini Japan, Tetsuji Umada, amefanya ziara katika kiwanda cha bia cha TBL kilichopo Ilala jijini ambapo alijionea shughuli za uzalishaji zinazoendeshwa na mifumo ya kisasa na teknolojia za hali ya juu na  kusema kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana na sekta ya viwanda inaweza kukuza uchumi wa Tanzania kwa haraka.

No comments :

Post a Comment