Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya SUNSHINE
GROUP, Betty Mkwasa wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa
Sunshine Mining Limited uliopo Chunya Agosti 1, 2017
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Dennis Dillip ambaye ni
Mjiolojia kuhusu mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni ya Sunshine
Mining Limited uliopo Chunya wakati alipoutembelea Agosti 1, 2017
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakipata
Maelezo kutoka kwa Afisa Madini wa Mkoa wa Mbeya Mhandisi Said
Mkwawa kuhusu taarifa za Kampuni ya Sunshine Gold Mininga Limited
wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni hiyo wilayani
Chunya Agosti 1, 2017
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia wimbo maalum unaozungumzia utendaji wa
serikali ya Awamu ya Tano ulioimbwa na Kwaya maarufu ya
Kiwete katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye
uwanja wa Sabsaba mjini Chunya Julai 1, 2017
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba
mjiini Chunya Agosti 1, 2017. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa
Mbeya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Kigoda kutoka kwa Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaso ikiwa ni ishala ya kusimikwa kuwa Chifu wa makabila ya Wasafwa na Wakimbu katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Chunya Agosti 1, 2017.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU ATEMBELEA MTAMBO WA KUSAFISHA DHAHABU CHUNYA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea
na kujionea mtambo wa kisasa wa kusafisha dhahabu kwa asilimia 99
unaomilikiwa na kampuni ya Sunshine Group uliopo katika kata ya Matundasi
wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Ametembelea mtambo huo leo (Jumanne,
Agosti 1, 2017) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya na kusema
kuwa mtambo huo ni wa kwanza kuweza kusafisha dhahabu kwa kiwango hicho hapa
nchini.
Amesema kwa Tanzania kampuni ya
Sunshine Group ndiyo yenye mtambo wa kuweza kusafisha dhahabu na kufikia
asilimia 99 ukilinganisha na makampuni mengine yanayomiliki migodi.
Pia Waziri Mkuu amesema Serikali
inaendelea kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza
katika mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia makinikia ili kuweza
kusafirisha dhahabu halisi.
Naye Ofisa Madini Mkoa wa Mbeya,
Mhadisi Said Makwama amesema dhahabu inayosafishwa katika mtambo huo ikipelekwa
nje ya nchi inaingizwa sokoni moja kwa moja tofauti na migodi mingine.
Mhandisi huyo alisema Sheria mpya ya Madini imesaidia Serikali kupata kodi ya juu
itokanayo na Mrabaha wa asilimia 6 na ‘clearance and inspection fee’ ya
asilimia moja ya thamani ya madini yanayosafirishwa ukilinganisha na
mrabaha wa awali wa asilimia nne.
“Uzalishaji uliofanyika kwa mwezi Julai tu
Serikali imepata mrabaha wa sh. milioni 333 ukilinganisha na sheria ya zamani
Serikali ingepata shilingi milioni 191. Sheria mpya imewezesha Serikali kupata
mapato zaidi ya sh. milioni 142. Awali ilikuwa inapata sh. milioni 191
kwa gramu 52. 518 kwa mgodi mmoja wa Sunshine.”
Kwa upande wake mbunge wa Chunya,
Mheshimiwa Victor Mwambalaswa ameiomba Serikali kukubali maombi ya Kampuni ya
Sunshine ya kujenga mtambo wa kuchenjulia mabaki ya mchanga wa dhahabu wilayani
Chunya ili kuweza kuongeza fursa za ajira, ambapo Waziri Mkuu amesema suala
hilo linashughulikiwa.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Sunshine Group Bw Leo Le alisema kampuni
ya Sunshine Group ni ni miongoni mwa makampuni makubwa kutoka nchini China
yaliyowekeza Tanzania, ambapo thamani ya uwekezaji wao ni zaidi ya Dola za
Marekani milioni 100.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 1, 2017
No comments :
Post a Comment