Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe
akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha walioagwa leo kwa ajili ya
kwenda nchini Uingereza katika mashindano ya London Marathon
yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa nane.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe
akizungumza wakati alipokabidhi bendera ya taifa kwa wachezaji 8 wa
Riadha walioagwa leo kwenda kwenye mashindano ya riadha ya London
Marahon yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa nane nchini Uingereza, Hafla
ya kuwaaga wachezaji hao imefanyika Hyatt Kilimanjaro Hotel jijini Dar
es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe akimkabidhi bendera ya taifa mwanariadha Alphonce
Felix Simbu kwa niaba ya wenzake katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika
leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Multchoice
Tanzania Bw. Maharage Chande na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania na
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe akishuhudia wakati Rais wa Chama cha Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akipongeza mwanariadha Alphonce Felix Simbu kwa niaba ya wenzake mara baada ya kukabidhiwa bendera ya taifa katika
hafla ya kuwaaga iliyofanyika leo jijini Dar es salaam Hyatt
Kilimanjaro Hotel , kutoka kulia Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari
Bw. Yusuph Singu na Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage
Chande.
Mwanariadha Alphonce
Felix Simbu akizungumza wakati alipokuwa akiwashukuru Multchoice kwa
kumpa ufadhili na kufadhili pia maandalizi ya kambi ya timu ya taifa ya
riadha wakati wa hafla hiyo.
Rais wa
Chama cha Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka
akimshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harisson
Mwakyembe, Multchoice pamoja na Jeshi la Wananchi kwa jinsi ambavyo
wamejitoa na kusaidia timu ya taifa ya Riadha na kwamba kazi iliyobaki
ni kuleta mafanikio katika mashindano yaliyo mbele yetu.
Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande
akizungumza katika hafla hiyo kama mdhamini wa timu hiyo kwa sasa
ambapo amewaomba makampuni mengine kushiriki katika kuidhamini timu ya
taifa ya Riadha ili kuleta mafanikio zaidi.
Kulia ni Meneja Mahusiano Multichoice Tanzania, Johnson Mshana na Shumbana Walwa Afisa Masoko Multchoice wakiwa katika hafla hiyo.
Meneja Mahusiano Multichoice Tanzania, Johnson Mshana akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanariadha wakitambulishwa katika hafla hiyo ya kuwaaga iliyofanyika leo Hyatt Kilimanjaro Hotel jijini Dar es salaam.
No comments :
Post a Comment