Mthamini wa ardhi kutoka ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Singida Chiku Mkina (aliyevaa miwani) na wataalaamu
wengine wakisikiliza kwa makini mada katika kikao kilichohusu uthamini
wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la
Kutoka Uganda hadi Tanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt
Angelina M Lutambi akichangia mada katika kikao kilichohusu uthamini wa
mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la
Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mkurugenzi wa kampuni ya Dighy
Welly Dkt Jan Perold akiwasilisha mada katika kikao kilichohusu uthamini
wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la
Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mwakilishi wa Serikali katika
zoezi la Uthamini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Linus Kinyondo
akizungumza na wataalamu wa mkoa wa Singida katika kikao kilichohusu
uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la
mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mhandisi wa Ujenzi wa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Singida Simwela Nuru Martin akifuatilia kwa makini kikao
kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi
wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
…………………….
Wananchi Mkoani Singida
wameondolewa wasiwasi kuhusu fidia ya mali au ardhi yao ambayo itapitiwa
na mradi wa bomba la mafuta kutoka ...Uganda hadi Tanga kwakuwa
hawatapunjwa bali itazingatia vigezo vya kimataifa na kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias
Tarimo amesema hayo mapema leo wakati wa kikao na wataalamu wanaofanya
uthamini wa mali na ardhi ambayo itapitiwa na mradi huo.
Tarimo amesema wananchi na taasisi
zote wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutaja gharama kulingana na
thamani halisi ya mali zao na sio kuongeza gharama za juu kwakuwa vigezo
vya kitaifa na kimataifa vitazingatiwa.
“wananchi wengine wasio waaminifu
wananweza wakataja pesa kubwa au hata kuvamia maeneo ambayo siyo yao
ilimradi wapate tu pesa, nawasihi wasifanye hivyo kwakua watakuwa
wanakwamisha mradi huu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu na
majirani zetu Uganda”, amesema na kuongeza kuwa
“ Tunampongeza na kumshukuru Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John P Magufuli kwa kuhakikisha
nchi yetu inapata mradi huu, tutoe ushirikiano wa kutosha ili mradi
ufanikiwe kw kiwango kikubwa hasa kwa maeneo yote utakapopita kwa Mkoa
wa Singida”, amesisitiza.
Tarimo ameongeza kuwa serikali ya
Mkoa, wilaya, taasisi na wananchi wote wa Singida wamekuwa mstari wa
mbele kutoa ushirikiano kwa miradi yote ya kitaifana kimataifa na hivyo
basi wataalamu wanaofanya uthamini na wale watakaokuja kujenga wasiwe na
wasiwasi wowote.
Ameongeza kuwa wananchina taasisi
ziko tayari kunufaika na mradi huo kupita Mkoani Singida kwa kupata
ajira za muda mfupi na mrefu, kufanya biashara pamoja na kutoa huduma
mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa
wa Singida Dkt Angelina M Lutambi amewataka wataalmau hao kushirikiana
na wataalamau wa ngazi zote kuanzia mkoa hadi vijiji ili zoezi la
uthamini liende vizuri.
Dkt Lutambi amesema lengo la
uthamini ni kuhakikisha wananchi hawapati madhara makubwa kutokana na
kupita kwa mradi huo katika maeneo hayo pamoja na kuhakikisha sheria,
miongozo na taratibu zote zinafuatwa.
Ameongeza kuwa wataalamu wanapaswa
kuwa wazi kwa kushirikisha taasisi na mashirika ambayo kwa namna moja
au nyingine yataguswa na mradi huo pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa
wakati kwa wote wanaohusika.
Wakichangia mada katika kikao
hicho wataalamu kutoka Mkoa wa Singida wamesema uthamini uangalie athari
zote ambazo zinaweza kutokea kutokana na mradi huo mfano athari ya
kisaikolojia ya usumbufu wa kumhamisha mtu kutoka katika makazi yake
pamoja na thari za maeneo kama vyanzo vya maji ambapo bomba litapita.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akizungumza katika kikao na wataalamu watakaofanya uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga. |
No comments :
Post a Comment