JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
IDARA YA UHAMIAJI
TAARIFA KWA UMMA
KUZINDULIWA KWA HUDUMA YA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI MTANDAONI (ONLINE PASSPORT APPLICATION FORM)
Idara ya Uhamiaji inapenda
kuutangazia umma kuwa imezindua rasmi huduma ya fomu ya maombi ya
pasipoti mtandaoni (Online Passport Application Form). Huduma hii
inapatikana katika tovuti ya Idara kupitia link ifuatayo: https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ na itaanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 07 Agosti, 2017.
Kufuatia kuzinduliwa kwa huduma hii, waombaji wote wa pasipoti wanashauriwa kuzijaza fomu hizo mtandaoni, Kisha kuzichapisha (Printing) na kuziwasilisha katika Ofisi za Uhamiaji.
Hata hivyo, matumizi ya huduma
hii yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya
pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo.
Utaratibu wa namna ya kujaza
fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja
wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia
anuani ya Idara ambayo ni info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao.
Taarifa zaidi kuhusu huduma hii zitaendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Imetolewa na:
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
04 AGOSTI, 2017.
Thanks so much for this information. I have to let you know I concur on several of the points you make here and others may require some further review, but I can see your viewpoint.
ReplyDeleteGHANA PASSPORT ONLINE