| Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. George B. Simbachawene akitoka kukagua jengo la madarasa mawili shule ya sekondari Loiborsiret wilayani Simanjiro mkoani Manyara alipofanya ziara mkoani humo jana |
Waziri wa Nchi OR TAMISEMI Mhe.
George B. Simbachawene akipatiwa maelezo kutoka kwa Mkuu wa shule ya
sekondari Loiborsiret wilayani Simanjiro mkoani Manyara juu ya ujenzi wa
madarasa ya shule hiyo ikiwemo ushiriki wa wananchi katika kuchangia
juhudi za Serikali.
Mhe.
George B. Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na walimu, wazazi na
uongozi wa wilaya ya Simanjiro mbele ya jengo la maabara shule ya
sekondari Loiborsiret ambalo ujenzi wake umevuka asilimia 60
Mhe.
George B. Simbachawene akikagua maendeleo ya kazi za mmoja wa wanafunzi
katika shule ya sekondari Loiborsiret wilayani Simanjiro mkoani Manyara
alipofanya ziara mkoani humo kujionea hali halisi ya maendeleo ya sekta
za elimu.
Mhe.
George B. Simbachawene akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za tatu za
walimu ambao umekamilika kwa asilimia mia moja, Mhe. Waziri alipongeza
kazi hiyo ya ujenzi na kuwataka Halmashauri nyingine kufuata mfano huo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki
mkutano wa kutafuta suluhu katika mgogoro wa kugombania kitongoji
kinachoitwa Katikati ambao vijiji vya Kityangale na Sukuro kila kimoja
kinakitaka kitongoji cha Katikati kiwe upande wake. Mgogoro huo umedumu
kutoka mwaka 2009
Mhe.
George B. Simbachawene mwenye dhamana na mamlaka ya Serikali za Mitaa
akizungumza na kutoa njia ambazo wananchi wa vijiji vya Sukuro na
Kityangale wanaweza kutumia kuhusu kutatua mgogoro wao wa kugombea
kitongoji cha Katikati unaweza kumalizwa. Mhe. Waziri alisisitiza kutoa
maoni kwa kujali mahitaji ya watu na sio kundi au makundi ya watu
Fulani.
……………………………………………………………………………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene
amepokea maoni ya wananchi wa vijiji vya Sukuro na Kityangale kwa ajili
ya kutoa suluhu ya mgogoro wa kitongoji cha Katikati kinachogombewa na
pande hizo mbili tangu mwaka 2009.
Akitoa maelezo ya awali Mhe.
Simbachawene amesema uamuzi wa Serikali utazingatia maslai ya wananchi
na nchi kwa ujumla na sio maslai binafsi kama ambavyo makundi makundi
yalivyo katika mgogogoro huo wa muda mrefu ambao hauna tija kwa wananchi
na maendeleo yao.
“Mimi nimeona na ninachukua maoni
yenu bila hata ya kupiga kura, na sitaki kusema nani ameshinda, sawa
jamani, acha niende, nitafakari, na nitarudisha majibu ndani ya siku
kumi na nne na majibu hayo yatakuwa ndiyo ya mwisho”
Amesema serikali haiwezi kubaki
kimya na haiamui, lakini uamuzi wa suala hili utazingatia sana maslai
mapana ya wananchi, shughuli za wananchi na Taifa kwa ujumla wala
hautaunga mkono kikundi fulani cha watu.
Aidha, alisema uamuzi wa
kitongoji cha katikati utazingatia zaidi kuwepo kwa amani na usalama wa
eneo lenyewe ili waweze kufanya shughuli za maendeleo na wao wenyewe kwa
ujumla.
“Jambo hili ni lazima liishe na
litaisha mapema sana, nitakuja kulisema hapa na ndio utakuwa uamuzi wa
Serikali. kwa hiyo, mimi nimepokea, uamuzi utakuja ndani ya siku kumi na
nne wenye maslai ya watu na maslai ya nchi kwa ujumla,”alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Manyara Mhe. Joel Bendera amesema ugawaji wa mipaka mipya ya maeneo hayo
itazingatia amani na utulivu kwani historia huko nyuma inaonyesha kuwa
kulikuwa na ugomvi ambao hauishi na kuwataka wananchi kusubiri uamuzi wa
mwisho wa Serikali.
Mgogoro wa kugombewa kitongoji
cha katikati ni wa muda mrefu kwani hata mipaka yake haijawekwa wazi kwa
kuwa mazingira ya Maafisa Ardhi kwenda kupima yamekuwa magumu na
wameshindwa kwa kuwa jamii hiyo kijiji cha Sukuro, Kityangale na
kitongoji cha katikati inayoishi hapo haitoi ushirikiano wa kuonyesha
mipaka halisi ya kitongoji hicho ili kila mmoja abaki na eneo kubwa
ijapokuwa kitongoji kina eneo kubwa la kutosha kuwa kijiji.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene ametembelea shule za
sekondari wilayani Simanjiro Loiborsiret na kujionea ujenzi wa nyumba za
walimu, madarasa na maabara ambao umefanikiwa kwa kiwango kikubwa na
mwisho alitembelea shule ya sekondari Emboreet yenye kidato cha tano na
kuahidi kuwaongezea idadi ya wanafunzi ndani ya muda mfupi.
Pia akiwa shuleni Emboreet
ameongea na wazazi, walimu na wanafunzi na kuwapongeza kwa kazi nzuri
wanayoifanya iwepo ya marafiki wa Shirika la ECLAT Foundation ya
Tanzania na Upendo society ya Ujerumani, wakiwemo Foundation for Care
and education ya Germany waliotoa fedha za kujenga majengo mbalimbali ya
shule hiyo kama shumba za wal;imu na maabara.
Waziri Simbachawene amehitimisha
ziara wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa kuiagiza mikoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali kuendelea kupanda miti na
kutunza mazingira kwa maslai ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment