Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua jambo kwa Eng,
Emmanuel Raphael Wansibho Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Viwanja vya
Ndege huku Meneja Ujenzi wa Kampuni BAM inayojenga uwanja huo ya Eng.
Ray Blumrick (kulia), akifuatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akiangalia ramani ya
namna muonekano wa miundombinu ya jengo la tatu la abiria litakavyokuwa
mara baada ya ujenzi wake kukamilika (kulia), ni mtaalaam wa ramani toka
kampuni ya BAM ya Uholanzi inayojenga uwanja huo akifafanua.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo ya
ujenzi wa jengo la tatu la abiria unavyoendelea kutoka kwa Meneja Ujenzi
wa Kampuni ya BAM inayojenga uwanja huo Eng. Ray Blumrick (kushoto),
ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baadae mwakani umefikia asilimia 64
ya ujenzi wake na utahudumia abiria milioni sita kwa mwaka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo ya
ujenzi wa jengo la tatu la abiria unavyoendelea kutoka kwa Meneja Ujenzi
wa Kampuni ya BAM inayojenga uwanja huo Eng. Ray Blumrick (kushoto),
ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baadae mwakani umefikia asilimia 64
ya ujenzi wake na utahudumia abiria milioni sita kwa mwaka.
…………………………..
Na Neema Harrison, TUDARCO
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof.
Makame Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la tatu la abiria
la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo sasa
utakamilika Oktoba 2018.Mhe. Prof. Mbarawa aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya mradi huo ulianza 2013, na sasa kuridhishwa na hatua waliyofikia.
Akizungumza mara baada ya kukagua
ujenzi huo, Prof. Waziri Prof. Mbarawa amesema kwa sasa ujenzi umefikia
asilimia 64, na hatua iliyobaki ni ujenzi wa wa mifumo ya ndani ya
jengo.
“Sote tumekuwa mashahidi nimekuwa
nuikitembelea mara kwa mara ujenzi wa jengo hili na ninaridhika kwa kasi
ya ujenzi wake, ambapo sasa tumefikia kwenye hatua nzuri na vitu
vilivyobaki sio vikubwa kama ilivyokuwa wakati wanaanza, hivyo ni
matumaini yangu hadi Oktoba mwakani (2018) jengo lote litakuwa
limekamilika na serikali kukabidhiwa,” amesema Mhe. Prof. Mbarawa.
Hatahivyo, Prof. Mbarawa amesema
serikali inatarajia kupata watalii wengi na serikali itapata mapato
kupitia kodi na tozo za abiria wanaosafiri kutumia kiwanja hiki, pia
wapangaji wanaotoa huduma mbalimbali yakiwemo maduka na usafiri wa
magari.
Amesema serikali itaendelea kutoa fedha za ujenzi wa jengo
hilo linalosimamiwa na mkandarasi BAM International ya Uholanzi, ambapo
pia likikamilika litatoa ajira kwa Watanzania wengi.“BAM wamekuwa wakifanya kazi nzuri nawapongeza sana na tunatarajia hadi kukamilika tutapata mradi bora utakaoliingizia taifa faida kubwa kutokana na kodi na tozo mbalimbali,” amesema Prof. Mbarawa.
Amesema jengo hilo likikamilika
linatarajia kuchukua abiria milioni sita (6) kwa mwaka, na kupunguza
msongamo ulipo katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII)
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment