Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WAZIRI
wa mambo ya ndani ya nchi ,Mwigulu Nchemba ,amewataka askari wa
uhamiaji nchini kuhakikisha wanataifisha magari na vyombo vya usafiri
wanavyokutwa navyo wahamiaji haramu ,wakati wanapokamatwa.
Aidha amewaagiza askari hao kuwakamata watu wanaowalipia faini wahamiaji haramu na
kuwafungulia mashitaka.Mwigulu aliyasema hayo,wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ofisi mpya ya uhamiaji ya mkoa wa Pwani ambazo zote zipo wilayani Kibaha.
Alisema endapo magari na vyombo vinavyosafirishia wahamiaji haramu ikiwemo boti vitaifishwe na kutumika katika kazi za ujenzi wa taifa.
“Haiwezekani mtu aingie nchini kwa
makusudi ,bila kibali halafu inapotakiwa kulipa faini kutokana na kosa
hilo atokee mtu kuwalipia faini kwa haraka jambo linalosababisha vitendo
hivyo kuenea kwa kasi”alisema Mwigulu.
Mwigulu
alieleza kwamba,ni lazima iangaliwe,jamii inapaswa kujiepusha na
kushirikiana na kundi hilo ili kupunguza wimbi kubwa la wahamiaji haramu
nchini.
Waziri huyo alisema ,iangaliwe
njia za kudhibiti wahamiaji hao pale inapotokea kukamatwa ama
kushtakiwa na kuhukumiwa pasipo kuwalinda kwa kuwalipia faini.
“Mkiwakamata
pia na magari myataifishe siku hiyo hiyo na kuyapeleka magereza ili
yakabebe mawe,na hata mkiwakamata kwenye boti taifisheni hizo boti
hakuna kuweka viporo”alisema Mwigulu.
Awali akitembelea ofisi mpya katika jengo la vitambulisho vya taifa
(NIDA),Mwigulu aliwaagiza watendaji wa ofisi hiyo kuhakikisha wanafanyia
kazi agizo la dk.John Magufuli la kuunganisha utambulisho wa jumla kwa
wananchi.“Wananchi wanatakiwa wawe na utambulisho wa aina moja pekee unaojumuisha taarifa zao zote”alisema alisisitiza Mwigulu.
Nae afisa Uhamiaji Mkoani Pwani ,Plasida Mazengo alisema ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vitendea kazi hali inayosababisha kufanyakazi kwenye mazingira magumu .
Alimuomba
waziri huyo kuangalia namna ya kusaidia kutatua changamoto hizo ili
waweze kufanya kazi zao kifanisi zaidi kwa maslahi ya watanzania.
Kaimu mkurugenzi wa uzalishaji vitambulisho (NIDA) Alfonce Malibiche alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 99.9 .
Kaimu mkurugenzi wa uzalishaji vitambulisho (NIDA) Alfonce Malibiche alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 99.9 .
Na utakapokamilika utawarahisishia wananchi kupata huduma kirahis,na jengo litaanza kazi rasmi mwishoni mwa mwezi huu .
No comments :
Post a Comment