Wednesday, August 2, 2017

MTANDAO WA ELIMU TANZANIA, (TenMet), WAKUTANA NA BLOGGERS JIJINI DARES SALAAM

Afisa Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bi. Alistidia Kamugisha, akizungumza wakati wa kikao cha kujenga ushirikiano baina ya taasisi hiyo na Bloggers kilichofanyika makao makuu ya TenMet, Sinza jijini Dar es Salaam, leo Agosti 2, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BINADAMU ili aweze kuyakabili mazingira yake, moja ya nyenzo muhimu ni elimu, na kwa kutambua umuhimu wa elimu, wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya juhudi kubwa katika kusaidiana na serikali ili kufikia lengo la kuwapatia elimu Wananchi wa Tanzania.
Mtandao wa Elimu Tanzania, kwa kifupi TenMet, ni moja ya taasisi zinazifanywa juhudi kub wa katika kuhakikisha malengo yaliyotajwa hapo juu yanafikiwa.
TenMet ambayo iliasisiwa miaka 18 iliyopita ikiunganisha taasisi nyingine 39 wakati huo, kwa sasa mtandao huo umepanuka na kufikia jumla ya taasisi 181 zilizojikita katika swala la kuhakikisha watanzania wanapatiwa haki yao ya elimu, lakini sio tu kupatiwa elimu bali pia elimu iliyo bora.
Ili kufikisha ujumbe kwa wahusika (jamii) TenMet hufikisha ujumbe kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na makongamano, semina na vyombo vya habari vikiwemo vile vya kisasa (social media kama vile Blogs).
Agosti 2, 2017, Maafisa wa TenMet waliwaalika bloggers ili kuangalia namna gani wanavyoweza kushirikiana katika kutekeleza malengo yaliyoanishwa hapo juu ya kusambaza taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya elimu.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, alisema, lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa kikazi baina ya taasisi yake na vyombo vya habari vya kimtandao kwani anaamini taarifa zitawafikia wadau wengi zaidi.
“Lakini pia tunaamini ushirikiano huu utatusaidia katika kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini, kwa kuhabarisha umma, hivyo tunayo furaha kubwa kukutana nanyi leo hii.”Alifafanua.
Kwa upande wake, Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha, amefafanua kuwa, TenMet kama ambavyo malengo yake yalivyoainishwa, imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali kuhusu elimu hapa nchini, lakini pia kwa kushirikiana na taassi nyingine za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuratibu mikutano, maonesho na semina kuhusu masuala ya elimu.

Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, (katikati), akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Bi. Alistidia Kamugisha, na Afisa Programu wa taasisi hiyo, Bw. David Sizya.
 Mmoja wa washiriki Bi.Victoria Mndeme wa Ayo Tv, akitoa maoni yake.
 Afisa wa TenMet, Bw. Dominic Dogani, akitoa ufafanuaiz wa masuala mbalimbali yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho.
 Majadiliano yakiendelea.

 Mmoja wa washiriki wa kikao akitoa maoni yake.
 Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakinakili yaliyokuwa yakijadiliwa kupitia vitendea kazi vyao.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), Bw. Joachim Mushi, akiwa makini na yaliyokuwa yakijadiliwa.
 Mmiliki wa blog ya Jiachie, Bw. Ahmad Michuzi (kulia) akifuatilia mjadala. Kushoto ni Bw. Mushi.
 Bi. Kamugisha akiweka sawa vitabu vyenye taarifa za TenMet.
 Bw. Sizya, (kulia), akimpatia nakala ya vitabu vya TenMet mwandishi wa Mo Blog, Bw. Rabif Humwe.
Picha ya pamoja

No comments :

Post a Comment