Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe akitoa nasaha zake kwenye kongamano la vijana wa kanisa Katoliki jimbo la Singida lililolenga kuwaelimisha vijana hao umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla. |
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa
wa Singida, Mhe. Aysharose Matembe, akipeana mikono na Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la
Singida, Edward Mapunda wakati wa kongamano la kuelimisha vijana wa
kanisa katoliki jimbo la Singida kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa
maendeleo ya Taifa.
Baadhi ya vijana Kanisa Katoliki
Jimbo la Singida waliohudhuria kongamano la wiki moja, lililofanyika
kwenye jukwaa la Askofu Mabula mjini Singida.
Baba Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo
la Singida, Edward Mapunda akizungumza kwenye kongamano la juma la
vijana wa katoliki hilo mkoani Singida. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa
Singida Aysharose Mattembe.
(Picha/habari na Nathaniel Limu).
………………………
Mbuge Viti Maalum (CCM) Mkoa wa
Singida, Aysharose Mattembe, amelipongeza kanisa la Katoliki jimbo la
Singida kwa uamuzi wake wa kuwaelimisha vijana 490 kuhusu umuhimu wa
kulipa kodi.
Mattembe ametoa pongezi hizo
wakati akizungumza kwenye ...kongamano la vijana waumini wa kanisa hilo
lililofanyika kwenye jukwaa la askofu Mabula kwenye viwanja vya kanisa
katoliki mjini hapa.
Amesema vijana wakiwezeshwa
kutambua mapema umuhimu wa kulipa kodi na manufaa yake, nchi itakuwa ya
walipa kodi ambao watalipa kwa hiyari yao bila kushurutishwa.
“Suala la kulipa kodi ni muhimu
mno kwa maendeleo ya nchi yo yote hapa duniani. Rais wetu Dkt Magufuli
ameleta mageuzi makubwa mno yanayohusu kulipa kodi. Anajua umuhimu wa
kulipa kodi kwa sababu bila kodi hakuna maendeleo. Baba Askofu, kitendo
chenu cha kutoa elimu ya kodi kwa vijana hawa mtakuwa mmemuunga mkono
rais Magufuli na hongereni sana”, amesema Mattembe.
Mbunge huyo amewataka vijana hao
ambao wametoka wilaya zote za mkoa wa Singida,wakawe mabalozi wazuri
katika kueneza elimu ya kulipa kodi kwa wenzao ambao hawakubahatika
kuhudhuria kongamano hilo.
“Vijana wenzangu haya maendeleo
makubwa mnayoyaona ya barabara nzuri, vituo vya afya na visima vya maji
na maengine mengi, yote yanagharamiwa na fedha za kodi na si vinginevyo.
Serikali ya awamu ya tano inamtaka kila mtanzania mwenye sifa ya kulipa
kodi alipe, tena kwa wakati bila ya kushurutishwa”, amesisitiza.
Aidha amaewataka vijana wote
mkoani hapa wenye sifa ya kufanya kazi, wajiunge kwenye vikundi vya
ujasiariamali pamoja na vile vya kilimo cha biashara, ili waweze
kujiletea maendeleo na kujikomboa kiuchumi.
“Faida za kujinga kwenye vikundi
vilivyosajiliwa ni nyingi ikiwemo ya kupata mikopo kwa masharti nafuu
kutoka taasisi za kifedha. Tunayo maeneo ya kutosha kwa ajili ya ufugaji
nyuki. Mazao ya nyuki yana soko kubwa ndani na nje ya nchi. Anzisheni
vikundi vya ufugaji nyuki mtaharakisha kujikomboa kiuchumi. Nina uhakika
serikali ya mkoa na ofisi yangu tutawasaidia ili muweze kufikia malengo
yenu”, amesema.
Mattembe ameahidi kuchangia
mizinga ya kisasa ya kutosha kwa vijana watakaojiunga katika vikundi
huku akiungwa mkono na Katibu wa Jumuiya ya Wanawake (CCM) Manispaa ya
Singida Magreth Malecela ambaye ameahidi kuchangia mizinga mitano ya
kisasa.
Awali Baba askofu wa jimbo la
Singida Edward Mapunda amesema vijana hao pia wamepewa elimu juu ya
ujasiriamali, kilimo cha biashara na maadili mema.
Aidha, amesema kongamano hilo
ambalo linafanyika kila mwaka mara moja, linatarajia kupanua wigo kwa
kupata wawezeshaji wa fani mbalimbai kutoka nje ya mkoa.
No comments :
Post a Comment