Mbunge
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwapa akina mama waliojifungua
mabeseni kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa kinamama
wa jimbo la mufindi na wananchi wote wanotumie hospitali ya mafinga
mjini lakini mabeseni hayo yametolewa kwa msaada wa ubalozi wa kuwait
hapa nchini Tanzania.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na mmoja wa kinamama alifanikiwa kupewa msaada wa beseni.
Na Fredy Mgunda,Mafinga.
Mbunge
wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mabeseni mia moja kwa akina
mama waliopata watoto kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya Mafinga.
Mabeseni hayo yalikabidhiwa kwa kina mama waliojifungua na ambao wanatarajia kujifungua hivi karibuni hospitalini hapo.
Msaada huo wenye thamani ya kiasi cha shilingi... milioni nne, umetolewa na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini mapema wiki iliyopita.
`ndugu
zangu zawadi hii tumepewa na Balozi wa Kuwait hapa Nchini kwa ajili
yenu kina mama kama sehemu ya mwanzo wa ushirikiano kati ya Mafinga na
Ubalozi wa Kuwait' alisema Chumi.
Akifafanua, alisema kuwa msaada huo ni uthibitisho wa upendo alionao Balozi wa Kuwait hapa nchini kwa watu wa Mafinga.
`Mheshimiwa
Balozi Jasem Al- Najem hajawai kufika Mafinga lakini kwa upendo mkubwa
akasema, naomba hiki kidogo uwafikushie kina mama wa Mafinga' alisema
Chumi na kuongeza kuwa ushirikiano kwenye jambo dogo ndio mwanzo wa
ushirikiano wa mambo mengine makubwa.
Akishukuru
wakati wa kukabidhi msaada huo wa mabeseni, Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga alipongeza ushirikiano wa Mbunge na
wadau mbali mbali na kuwasihi watendaji kuendelea kufanya kazi kwa
kujituma.
`sisi
halmashauri tuko bega kwa bega na mbunge, na ninyi watumishi kwa pamoja
tuendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa kujituma' alisisitiza
Makoga.
Wakati
akikabidhi msaada huo wiki moja iliyopita kwenye ofisi za Ubalozi wa
Kuwait Masaki Jijini Dar es Salaam, Balozi Jasem Al-Najem alisema kuwa
lengo la Ubalozi ni kugawa jumla ya mabeseni elfu moja kwa ajili ya mama
na mtoto.
`katika
awamu ya kwanza ya kutoa msaada huu wa mabeseni haya ya mama mtoto
kits, tumeona tuwakumbuke na kina mama wa Mafinga japo kwa mabeseni mia
moja'
Ubalozi
wa Kuwait umekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii na
kibinadamu ambapo mpaka sasa wameshachimba visima arobaini kwenye shule
mbali mbali za Mkoa wa Dar na Pwani.
No comments :
Post a Comment