Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akiongoza
kikao kilichoshirikisha watendaji kutoka Kampuni inayojihusisha na
utafiti na uchimbaji wa gesi ya M & P Exploration Production
Tanzania Limited, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akizungumza na
Meneja Mkuu kutoka Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa
gesi ya M & P Exploration Production Tanzania Limited, Christophe
Maitre ( kushoto) katika kikao hicho.
Sehemu ya watendaji kutoka Wizara
ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa
yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho
…………………..
Leo Agosti 31, 2017 Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
amekutana na Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi ya M
& P Exploration Production Tanzania Limited kwenye Ofisi za Wizara
ya Nishati na Madini zilizopo jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni
kujadili namna ya kuendeleza gesi ya Mnazi Bay. Kikao hicho pia
kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC)
No comments :
Post a Comment