Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati)
akionyesha Jarida la Mpango Mkakati la Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT)
mara baada ya... kufanya nao mazungumzo katika Ofisi za Wizara 01 Agosti, 2017
Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA BENEDICT
LIWENGA-WHUSM)
NA
BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaana Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi
Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) kuwatatulia kero ya eneo la kufanyia
mafunzo pamoja na ofisi ambalo limekuwa likiwakabili kwa muda mrefu zikiwemo na
changamoto nyingine za Shirikisho hilo.
Mhe.
Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya
mazungumzo na baadhi ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa shirikisho hilo ikiwa
ni sehemu ya kutambua utendaji kazi wao na changamoto zinazowakabili ili ziweze
kutatuliwa.
Dkt.
Mwakyembe amesema kwamba, kutokana na tatizo la ukosefu wa eneo rasmi la ofisi
na sehemu ya kufanyia mafunzo, yeye atawasiliana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ili kuona namna gani wanaweza kupata
eneo kwa ajili ya kulisaidia shirikisho hilo kwa ajili ya kujenga ofisi na eneo
la kufanyia mazoezi.
Sambamba
na hilo, ameupongeza uongozi wa shirikisho hilo kwa kazi wanazozifanya na
kuwataka wazidi kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hususani
katika kupeana taarifa zinazohusu maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini.
“BFT jitahidini muwe na ushirikiano wa karibu na
Baraza la
No comments :
Post a Comment