Na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Waziri
Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameelekeza Baraza la Michezo Tanzania(BMT)
livunjwe na shughuli zake kufanywa na Sekretarieti hadi ...hapo Baraza
jipya litakapoundwa tena.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akisoma hotuba
ya kuhairisha mkutano wa saba wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
“Serikali
ya awamu ya tano haitafumbia macho usimamizi mbovu na utawala wa
michezo usiojali maslahi ya Taifa,Serikali imeazimia kuimarisha
utendaji kwa vyombo vya michezo nchini ili kila mwenye dhamana awajibike
ipasavyo”,Aliongeza Mhe.Majaliwa.
Aidha
katika hotuba yake amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dk John Pombe Magufuli kwa kuunga mkono jitihada za michezo nchini
kwa dhamira yake ya kujenga Uwanja mkubwa wa Michezo hapa mjini Dodoma
kwa kushawishi mataifa rafiki kama vile Moroco ambao wanajenga uwanja
huo.
Pia
amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa michezo kwa Afya,umoja wa
kitaifa na kama fursa ya ajira kwa vijana wetu ambapo ivi karibuni
mkoani Mwanza yamehitimishwa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA
yaliyoibua vipaji na hamasa kubwa iliyo miongoni mwa vijana nchini.
“Tutaendelea
kuratibu michezo shuleni,ikiwa ni pamoja na kusimamia ufundishaji wa
michezo kama somo,maelekezo yetu ni kwamba kila mkoa uwe na shule
angalau mbili zenye mchepuo wa michezo na walimu wenye sifa stahiki za
kufundisha michezo,Ameeleza Mhe.Majaliwa.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia ameipongeza kwa dhati timu ya Serengeti Boys kwa
kutoa upinzani mkubwa kwenye mashindano ya shirikisho la Mpira wa Miguu
Barani Afrika na kuweka msisitizo kwa Chama cha Mpira nchini(TFF)
kuendelea kuwatunza vijana hao.
“Msisitizo
wangu kwa TFF ni kuendelea kuwatunza vijana hao na kusimamia vilabu vya
michezo nchini, kuwekeza kwenye soka la vijana ili kujenga timu imara
kwa miaka michache ijayo”,Aliongeza Mhe.Majaliwa.
No comments :
Post a Comment