|
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Shule ya
Misingi ya Mwaka katika mji mdogo wa Tunduma. Alikuwa katika
ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017.
NA OWM, TUNDUMA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya
Mji wa Tunduma wilayani Momba kuanzisha mradi wa ujenzi wa hospitali.
Amesema sh. milioni 900 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa
ofisi ya Halmashauri kwa sasa zianze kutumika katika kuanzisha ujenzi wa
hospitali hiyo.
Agizo hilo alilitoa jana jioni (Ijumaa, Julai 21, 2017) wakati akizungumza na
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Shule ya Msingi
Tunduma.
“Kwa kuwa afya ni jambo muhimu katika utekelezaji wa kauli mbiu
ya Rais Dkt. John Magufuli ya Hapa Kazi Tu, hivyo naagiza fedha zilizotengwa
kuanza ujenzi wa ofisi zitumike katika ujenzi wa hospitali.”
Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuongezea sh.
milioni 126 katika ujenzi huo. Fedha hizo zilitengwa kwa ajili ya
kuwafidia wamiliki wa eneo lililotengwa awali kwa ajili ya kujenga hospitali,
ambapo aliwataka watafute eneo lisilohitaji fidia.
Pia, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA) iandae ramani kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo na kuhusu suala la
ujenzi wa ofisi Serikali italishughulikia.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya Mbunge wa jimbo la
Tunduma, Mheshimiwa Frank Mwakajoka aliyeiomba kuiomba Serikali kuwajengea
hospitali kwa kuwa halmashauri hiyo haina hospitali, hivyo kusababisha usumbufu
mkubwa kwa wananchi pale wanapohitaji huduma hiyo.
Naye Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Juma Irando alitaja baadhi ya
changamoto zinazoikabili wilaya hiyo kuwa ni ukosefu wa hospitali ya wilaya,
ukosefu wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ofisi za Halmashauri.
Pia changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu ya barabara
iliwemo ya Makamba-Ikana inayotakiwa kukarabatiwa inayounganisha ukanda wa juu
na chini ili wananchi wa ukanda wa juu waweze kufika makao makuu ya wilaya.
|
|
Baadhi
ya wananchi wa mji mdogo wa Tunduma mkoani Songwe wakimshangilia Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Uwanja wa Shule ya Misngi ya
Mwaka Julai 21, 2017. |
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipokagua eneo la ujenzi wa
jengo la pamoja la forodha kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia katika mji
mdogo wa Tunduma. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ujumbe kutoka kwa Chifu Jubeki Chimpansya wa
Momba baada ya kusimikwa na wazee wa mila kuwa Chifu Simpanji katika
mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye Uwanja wa Shule ya Misngi ya Mwaka
katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Songwe Julai 21, 2017.
|
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto kwake) wakitazama gari
lililotengenezwa na Adam Zachariah Kinyekie wakati alipowasili kwenye
uwanja wa Shule ya Misngi ya Mwaka katika mji Mdogo wa Tunduma kuhutubia
mkutano wa hadhara Julai 21, 2017. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa
Mbeya na Songwe, Erasto Zambi. |
|
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua wa Ujenzi wa banio na mfereji wa maji
wakati alipotembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Makamba wilayani Momba
Julai 21, 2017. |
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Dickson Mwandambila ambaye ni
mlemavu baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Shule ya
Msingi ya Mwaka katika mji mdogo wa Tunduma. Alikuwa katika ziara ya mkoa
wa Songwe Julai 21, 2017.
No comments :
Post a Comment