Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Profesa. Mohamed Janabi akipeana mkono na Kiongozi wa Msafara wa baadhi
ya Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara wakati wa ziara yao katika
Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Profesa. Mohamed Janabi akielezea jambo wakati wa ziara ya Wajumbe wa
Kamati ya Huduma za Jamii wa Bunge la Uganda waliotembelea Taasisi hiyo
leo Jijini Dar es Salaam. Wabunge hao wametembelea Taasisi hiyo ili
kujionea namna inavyofanya majukumu yake.
Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Mussa Zungu akizungumza jambo mbele ya Wabunge kutoka Uganda
walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar
es Salaam. Kutoka kushoto ni Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka
Uganda Mhe. Cecilia Barbara na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi (katikati).
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakifuatilia Maelezo kuhusu namna
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inavyofanya kazi wakati wa
ziara yao katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakiwa katika sehemu ya mapokezi ya
kuingia Wodi ya Watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
leo Jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment