Pages
Monday, July 31, 2017
UNCDF YAWEZESHA UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA BWAWA LA KALEMAWE
SERIKALI ya Tanzania, imeshukuru Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa
(UNCDF) kwa kuwezesha watanzania kupambana na umaskini kupitia miradi
wanayoidhamini au kuitafutia fedha.
Kwa miongo miwili UNCDF imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na
Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya rais Tawala za Mikoa na serikali
za mitaa (TAMISEMI) katika mpango wa kupeleka madaraka kwa umma na
shughuli za maendeleo ya kiuchumi .
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe katika hotuba yake iliyosomwa
na Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Aisha Amour kwenye ufunguzi wa
kongamano la siku 2 la Wadau wa Ufugaji Samaki Kibiashara Bwawa la
Kalemawe lililoko wilaya ya Same mwishoni mwa wiki.
“Tunafurahishwa kwa namna ya pekee na UNCDF kwa jitihada zake
zinazoendeshwa kupitia katika Mpango wa Ufadhili Miradi ya kiuchumi
(LFI),” alisema Iyombe na kuongeza:
“Tunapokutana hapa tunapewa fursa na kufunuliwa uzoefu wa ushiriki wa
UNCDF katika miradi mbalimbali, safari hii tukishuhudia hatua yake ya
kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa
Kilimanjaro.”
Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo
kuhusu mradi wa ufugaji samaki katika shamba hilo kwa viongozi
mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya
ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya
Bagamoyo. Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mh. Naghenjwa
Kaboyoka na Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki
pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (wa pili kulia).[/caption]
Pamoja na kushukuru kwa hatua mbalimbali zilizofikiwa na taasisi hiyo
katika kusaidia watanzania, aliwataka wakazi wa Same kuhakikisha kwamba
mradi huo ulioundiwa kampuni ili kwenda kibiashara unafanikiwa na kuwa
mfano kwa wengine.
Halmashauri ya wilaya ya Same, na jamii inayozunguka bwawa la Kalemawe
wanashirikiana na UNCDF kuboresha miundo mbinu ya bwawa hilo na
kuwezesha uwapo wa uwekezaji kwa kuanzisha kampuni.
Kampuni hiyo iliyosajiliwa ya Kalemawe Dam Investment Limited katika
mpango maalum (SPV) inamilikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Halmashauri
ya wilaya ya Same, halmashauri ya vijiji sita, wakala wa serikali, watu
binafsi pamoja na makundi ya kijamii.
Kuwapo
kwa kampuni hiyo ni juhudi zinazofanywa za kuwezesha uhusiano mahsusi
wa kibiashara unaohusisha ubia wa Serikali, Binafsi na jamii (PPCP) kwa
kutoa umiliki linganifu mpaka katika ngazi za chini za mamlaka za
kijiji, ambazo kimsingi ndizo wamiliki wa maliasili muhimu ya ardhi kwa
mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya Mwaka 1999.
Viongozi
mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) wakiwa kwenye ziara fupi ya mafunzo
kuhusu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba la ufugaji samaki la
Ruvu lililopo wilaya ya Bagamoyo.[/caption]
Mradi huo wa Ufugaji wa Samaki Kibiashara wa Bwawa la Kalemawe ni zao la
ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Same, Kata za Ndungu na
Kalemawe, asasi zisizo za kiserikali na wadau wa maendeleo walioazimia
kukarabati na kufufua bwawa hilo na mfumo wake wa kilimo cha
umwagiliaji.
UNCDF kwa kushirikiana na wabia wake waitwao Mikono Tayari (ambao ni
kundi linaloundwa na washirika kutoka Tanzania na Norway) ni wataalamu
katika mradi hu wa ufugaji samaki kwa pamoja na SPV ya Same na washirika
wake.
Katika kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya
Same Rosemary Staki amesema wilaya yake ipo tayari kutekeleza mradi huo
ambao una manufaa makubwa si tu kwa watu wa Kalemawe na vijiji
vinavyozunguka bali pia na halmashauri ya wilaya ya Same.
Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo
kuhusu vyakula vinavyotumika kulisha samaki wanaofugwa kwenye shamba
hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi
ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo
lililopo wilaya ya Bagamoyo.[/caption]
Akishiriki katika mjadala aliwataka wanakalemawe kutambua umuhimu wa
mradi huo na kwamba hicho ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa watu
binafsi na jamii kwa ujumla.
Mradi huo ambao ni sehemu ya programu kubwa ya kubadili watu wenye
makazi kuzunguka bwawa hilo umelenga katika siku za usoni kuzalisha
samaki na vifaranga vyake.
Ili kuwa na uelewa mkubwa wa kufanya biashara hiyo ya samaki, madiwani
na wenyeviti wa serikali za mitaa za vijiji vinavyotengeneza kampuni
hiyo ya Kalemawe walitembelea shamba la samaki Ruvu ambapo waliona
shughuli mbalimbali zinazoendelea katika shamba hilo ili iwe mfano kwao
Pamoja na kuuza samaki shamba hilo ambalo lipo kilomita 20 kutoka
Bagamoyo na kilomita 13 hivi kutoka Mlandizi linafuga samaki aina ya
sato na hutotolesha vifaranga laki moja kila wiki kwa kulingana na oda
zilizopo.
Ziara
ya mafunzo ikiendelea katika shamba la kufuga samaki la Ruvu lililopo
wilayani Bagamoyo. Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (wa pili
kushoto) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (katikati) pamoja na ujumbe
ulioambatana nao kwenye mafunzo hayo ukitazama jambo katika shamba
hilo.[/caption]
Mmoja wa viongozi katika mradi huo Khumbo Kanthenga alisema kwamba mradi
huo ambao bado unapanuliwa kufikia mabwawa sitini kwa sasa umelenga
kutoa vifaranga kwa mujibu wa oda na pia kuuza samaki ambao wapo tayari
kuingia sokoni samaki hao wanafikia gramu 350 na kuendelea.
Naye Mbunge wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka ambaye alikuwapo
katika kongamano hilo alielezea haja ya wananchi wengi kutambua mipaka
yao na kuhakikisha kwamba dhamira safi iliyopo ya kufufua bwawa hilo na
kubadilisha maisha ya wananchi inafikiwa.
Wakifunga
Kongamano hilo UNCDF ili shukuru ushirikiano mkubwa wa karibu ambao
umeonyeshwa na washiriki wa warsha hii ya wadau kuanzia serikali kuu,
mkoa, willaya na viongozi wa vijiji sita vinavyohusika na utekelezaji wa
mradi na pia iliahidi kua mashirika mengine ya umoja wa mataifa
watashirikishwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huu na miradi
mingine mbalimbali katika eneo hili la bwawa la samaki.
Eneo
ambalo linaandaliwa kwa ajili ya bwawa la kufugia samaki katika shamba
la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamayo.
Wafanyakazi
wa shamba la kufugia samaki la Ruvu wakitega nyavu kwa ajili ya
kuonyesha samaki katika moja ya mabwawa kwenye shamba hilo wakati wa
ziara hiyo fupi ya mafunzo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shamba hilo akiwa ameshikilia samaki aina Sato wanaofugwa kwenye shamba hilo.
Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (tisheti nyekundu) akitoa
maelezo katika chumba maalum cha kutotolea vifaranga vya samaki kwa
viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliokuwa kwenye ziara fupi ya
kupata elimu juu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo
lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Mshauri
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Per Gjoede akitazama mabwawa ya samaki
katika shamba la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamoyo.
Mkurugenzi
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Daudi Makobole (wa pili kulia)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (kulia)
pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (kushoto), Mshauri wa Shamba la
Samaki la Ruvu, Per Gjoede (wa pili kushoto) baada ya kuhitimisha ziara
fupi ya mafunzo katika shamba hilo.
Mkuu
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)
nchini, Peter Malika akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour
akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya siku mbilli ya wadau wa mradi
wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Same, Rosemary Staki.
Mkuu
wa wilaya ya Same, Rosemary Staki akitoa salamu kwa wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe wakati wa warsha
hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mwandamizi anayeshughulikia uwekezaji katika Shirika la Umoja wa
Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Imanuel Muro akisimamia
majadiliano kuhusu wa kampuni ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani
Same mkoani Kilimanjaro wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi
wa ufugaji samaki kibiashara katika bwawa hilo iliyoandaliwa na UNCDF
na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkiurugenzi
Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dr. Charles Mhina
akitoa maoni kwenye warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Misufini kata ya Ngungu wilaya ya Same, Omari Mganga
akiwasilisha maoni wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Mgandu kata ya Bendera wilaya ya Same, Merina Mhando
akichangia maoni katika warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu
wa Mawasiliano na Ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko
wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Jacqueline Namfua-Mwombela na
Mshirika wa Programu UNCDF, Andulile Mwabulambo wakifurahi jambo wakati
wa warsha hiyo iliyofanyika wmishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Pichani
juu na chini ni washirki wa warsha ya siku mbili ya mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyoandaliwa na UNCDF na
kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment