Saturday, July 1, 2017

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 57 YA UHURU WA CONGO ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM


unnamed
BALOZI wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, akizungumza wakati akisoma hotuba yake katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo jijini Dar es Salaam, juzi usiku. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Mambo ya Nje, Suleiman Saleh
1
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akisoma hotuba yake katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo jijini Dar es Salaam, juzi usiku. Katikati ni Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba (kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Mambo ya Nje, Suleiman Saleh
2
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) na Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, wakigonganisha Glasi ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya sherehe za miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, juzi usiku
3
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kushoto) na Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, kwa pamoja wakikata Keki ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya sherehe za miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, juzi usiku.
4
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) na Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, wakifurahia jambo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, juzi usiku.
5
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo wakibadilishana mawazo.
6
Baadhi ya Wakongo wakiimba wimbo wa Taifa katika sherehe hizo.
7
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea jukwaani katika maadhimisho hayo.
8
Mwanamuziki wa Kimataifa, kutoka Congo, Ferre Gola, akitoa burudani katika sherehe hizo.
9
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akicheza muziki na mwanamuziki Ferre Gola, wakati wa sherehe hizo.
10
Wanamitindo wakipita jukwaani kutoa shoo la onyesho la mavazi wakati wa sherehe hizo. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

No comments :

Post a Comment