Ujumbe wa wageni wakiangalia bia zinavyotengenewa kiwandani
Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga akielezea ujumbe miradi mbalimbali ya kijamii ya kampuni
Mtaalamu wa upishi wa bia wa TBL Group, Roseana Modest,akiupatia ujumbe huo maelezo kuhusiana na mchakato wa kutengeneza bia
Ujumbe wa wageni na maofisa wa TBL Group katika picha ya pamoja baada ya ziara
Mtaalam wa Ubora wa kiwanda cha bia cha TBL Jane Mwambuma (kushoto) akiwapa maelezo ya utengenezaji bia wageni waliotembelea kiwanda
……………………………………………………………………………….
Viongozi wa wanawake wa Vyama vya wafanyakazi kutoka nchini Zambia na viongozi wanawake wa vyama vya wafanyakazi kutoka nchini (TUICO) wamefanya
ziara ya mafunzo katika kiwanda cha TBL kilichopo jijini Dar es Salaa
na wamevutiwa na mkakati wa kampuni hiyo wa kuzingatia usawa wa jinsia
kwa kutoa fursa sawa za uongozi ndani ya kampuni ikiwemo jitihada za
kuwakwamua wanawake wasio waajiriwa kiuchumi katika utekelezaji wa... sera
ya kampuni mama ya ABInBev ya ‘Dunia Maridhawa’.
Akiongea
na ujumbe wa wanawake hao,Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga,
alisema mkakati huo wa kuzingatia usawa wa kijinsia unachangia kwa kiasi
kikubwa kampuni hiyo kuendelea kupata mafanikio makubwa katika nyanja
mbalimbali.
Zena Tenga, alisema kuwa kampuni inatekeleza
kwa vitendo sera ya kampuni yake mama ya kimataifa ya ABInBev ambayo
inatoa fursa sawa kwa wafanyakazi wake wote bila kujali jinsia ikiwemo
kuwapatia fursa za uongozi wafanyakazi
wanawake ndani ya viwanda vyake na sehemu nyinginezo za biashara zake
na wanaendelea kufanya vizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi hauna jinsia.
Alisema kampuni inalo jukwaa la wafanyakazi wanawake walioajiriwa na kampuni lijulikanalo kama TBL Women’s Forum ambalo
lengo lake kubwa ni kuwaunganisha wafanyakazi wote wanawake ndani ya
kampuni na kuwawezesha kubadilishana mawazo ya kukabiliana na changamoto
mbalimbali za kimaisha ikiwemo kuweka mikakati ya kujiendeleza katika
fani zao.
“Pamoja
na kuzingatia usawa wa kijinsia kampuni inao mkakati wa kuwaendeleza
wafanyakazi wanawake kielimu ambapo tayari baadhi ya wafanyakazi wamewezeshwa kuhudhuria na wamehitimu mafunzo ya ‘Mwanamke wa Wakati ujao’ yanayotolewa
na na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na taasisi ya
Confederation of Norwegian Enterprises (NHO)”alisema.
Tenga
aliueleza ujumbe huo mafakio mbalimbali ambayo kampuni imepata ikiwemo
kupata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya mwajiri bora nchini na tuzo ya
kimataifa ya Top Employers Award kutokana na utekelezaji wa kanuni za
raslimali watu kwa viwango vinavyokubalika kimataifa vilevile kutekeleza
miradi ya kuwasaidia akina mama kjikwamua kiuchumi mojawapo ukiwa ni
mradi wa Chibuku Mamas.
Akiongea kwa niaba ya wenzake,Brenda Mufika kutoka Chama cha wafanyakazi Migodini nchini Zambia,
alisema wamejifunza mambo mengi katika ziara yao kiwandani hapo na moja
ya suala kubwa lililowavutia ni kampuni kuzingatia usawa wa kijinsia
katika maeneo ya kazi,kuzingatia sheria za kazi za nchi pia kufanya
uzalishaji wa kutumia teknolojia za kisasa na rafiki kwa mazingira na
uzingatiaji wa hali ya juu wa kanuni za usalama mahali pa kazi.
Mufika alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kuwapatia wanawake nafasi ya kupata mafunzo ya kuwawezesha kushika nafasi za uongozi wa juu katika sehemu zao za kazi na
kwenye vyama vya kutetea maslahi ya wafanyakazi kwa kuwa dunia ya sasa
inahitaji elimu ya kisasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na
kuleta ufanisi katika sehemu za kazi
No comments :
Post a Comment