Mkurugenzi
wa TBL Group,Roberto Jarrin (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa
ABinBev kanda ya Afrika,Ricardo Tadeu,wakati alipofanya ziara ya kikazi
katika kiwanda cha Konyagi (TDL) kilichopo jijini Dar es Salaam,wengine
pichani wa kwanza kulia ni Meneja ubora wa kiwanda hicho, Asheri Magandi na Mhandisi Mwandamizi wa kiwanda hicho,Salvatory Rweyemamu.
Rais
wa ABInBev Africa,Ricardo Tadeu (wa pili kulia) akipata maelezo jinsi
mtambo mpya wa kuzalisha vifungashio vya vioo unavyofanya kazi kutoka
kwa Meneja Ubora wa kiwanda cha Konyagi,Asheri Magandi wakati alipofanya
ziara ya siku moja nchini jana.Wengine pichani ni Maofisa waandamizi wa
kiwanda hicho kilichopo jijini Dar es Salaam
Rais
wa ABInBev Africa,Ricardo Tadeu akitembelea eneo la mtambo wa
vifungashio vya kioo wa TDL na kupatiwa maelezo kuhusiana na uzalishaji
……………………
Ni utekelezaji wa sera ya kampuni ya Better World
Rais
wa kampuni ya mama ya TBL ya ABInBEV kanda ya Afrika,Ricardo Tadeu,
amefanya ziara ya siku moja nchini na kutembelea kiwanda cha TDLmaarufu
kama Konyagi kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo alijionea jitihada za
kiwanda hicho kufanya uzalishaji kwa kufuata kanuni za utunzaji wa mazingira.
Tadeu pia alipata fursa ya kutembelea mtambo mpya wa kuzalisha vifungashio vya vinywaji
vya kioo badala ya mifuko ya plastiki ukiwa ni utekelezaji wa agizo la
serikali la kupiga marufuku kuuza vinywaji vilivyofungwa kwa kutumia
mifuko ya plastiki maarufu kama viroba.
Mkurugenzi wa TBL Group na Mkuu wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin,alieleza jinsi TBL Group ilivyojipanga
kutekeleza kwa vitendo mkakati wa serikali ya awamu ya tano wa kuifanya
Tanzania kwa nchi ya viwanda sambamba na kuendesha viwanda kwa kutumia
teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.
“Tunafurahi
kuona serikali ya awamu ya tano inaweka msisitizo wa kujenga viwanda
nasi kama wawekezaji katika sekta hii tumejipanga kuendelea kuwa na
viwanda bora vinavyotumia teknolojia za kisasa na rafiki kwa
mazingira,kupunguza matumizi ya maji,kupanua wigo wa ajira kwa kufanya
kazi kwa kushirikiana na wakulima wanaotuuzia malighafi na kuchangia
pato la serikali kwa kulipa kodi”.Alisema Roberto.
Roberto
alieleza kuwa hivi sasa kampuni ya TDL ambayo iko chini ya TBL Group
imefunga mtambo wa kisasa wa kuzalisha vifungashio vya kioo ambao
utawezesha vinywaji vilivyokuwa vinafungwa kwenye vifungashio vya
plastiki kupatikana kwenye vifungashio vya kioo vyenye ubora,rafiki wa
mazingira na ambavyo sio rahisi kuigizwa na wafanyabiashara wasio
waaminifu kwenye masoko.
Mkurugenzi
huyo wa TBL Group alimhakikishia Rais huyo wa ABInBEV kuwa itahakikisha
inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali na wadau wote kuhakikisha
mkakati wa kufanya mapinduzi ya viwanda nchini unapata mafanikio na
kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hii.
No comments :
Post a Comment