Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,
Mhe. Benjamini William Mkapa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo
jipya la upasuaji kwenye kituo cha afya cha Nkomo kilichopo kijiji cha
Mwalushu,Wilayani Itilima-Simiyu
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima
Dkt. Anold Musiba akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu,kulia ni Balaozi wa
Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshida. Jengo hilo limejengwa na
Ubalozi wa Japan kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa na kugharimu kiasi
cha shilingi za kitanzania milioni 270.
Rais Mstaafu akiangalia moja ya
vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji .Ujenzi wa jengo hilo kwa
asilimia kubwa itawasaidia akina mama wajawazito ambapo awali wananchi
wa kijiji hicho walikua wakitembea kilometa arobaini kwenda kupata
huduma za namna hiyo.
hilo la upasuaji linavyoonekana
Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo
kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa Geofrey Nyaluke (mwenye fulana ya
jano) akitoa maelezo kwa Viongozi waliofika kushuhudia ufunguzi wa jengo
hilo
Rais Mstaafu akicheza mara baada
ya ufunguzi wa jengo hilo,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony
Mtaka na kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Daudi Njalu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu likiwahutubia wananchi wakati wa ufunguzi wa jengo la upasuaji wilaya ya Itilima.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria ufunguzi huo akiwepo mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa
Rais Mstaafu wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania wa awamu ya tatu akihutubia wananchi( hawapo
pichani),ambapo aliwataka Watanzania kuongeza hali ya kujiendeleza na
kujitegemea ili kutatua changamoto zinazowakabili ili kuweza kufufua
pamoja na kukuza uchumi wan chi.
Wananchi wa kijiji cha Mwalushu
wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa
jengo la upasuaji katika kituo cha afya cha Nkomo.(PICHA ZOTE NA WIZARA
YA AFYA)
No comments :
Post a Comment