Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Tellack, mara baada ya
kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
Meneja
wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoa wa Shinyanga Eng. Amosi Manyete akimuonesha
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, mfumo wa maji
taka uliowekwa nje ya jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Shinyanga
iliyopo mkoani humo. Kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda hiyo Mhe.
Jaji Richard Kibella.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua moja ya
nyumba za watumishi eneo la Rubaga zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA), mkoani Shinyanga.
Muonekano
wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga ambalo limekamilika na
ujenzi wake umesimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
NA
WUUM, SHINYANGA
WAZIRI
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha ndani ya miezi sita wanakamilisha ujenzi wa
nyumba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Prof.
Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani humo wakati alipokagua miradi mbalimbali
inayotekelezwa na Wakala huo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu
wa kuwapatia waheshimiwa majaji mahali pazuri pa kuishi ili waweze kutimiza
wajibu wao wa kutenda haki kwa wananchi ipasavyo.
“Hakikisheni
mnakamilisha ujenzi wa nyumba hii haraka iwezekanavyo ili Mheshimiwa huyu apate
mahali pazuri pa kuishi, kufanya hivi kutarahisisha majukumu yake na kufanikish
utendaji wa kazi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amesisitiza
umuhimu wa Wakala huo kuongeza kasi katika miradi mbalimbali inayoendelea ya
ujenzi wa nyumba za viongozi ili kuondoa adha ya kodi za pango kubwa
zinazopotea kwa viongozi hao kupanga kwa watu binafsi.
Naye,
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga Mhe. Jaji Richard Kibella amemshukuru
Prof. Mbarawa kwa niaba ya taasisi zake za TBA na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),
kwa namna ambavyo wameshirikiana na Mahakama kukamilisha ujenzi wa jengo hilo
na kuwapatia huduma nyingine za uendeshaji.
Aidha,
ameiomba Serikali kukamilisha kwa haraka ujenzi wa nyumba za viongozi na watumishi
wa mahakama kwani gharama kubwa zinatumika katika malipo ya upangaji wa nyumba
za viongozi.
“Mhe.
Prof. Mbarawa suala la nyumba ni changamoto, nyumba za kupanga zina gharama kubwa
ambapo kwa namna moja au nyingine inaongeza gharama za uendeshaji wa mahakama
na kupunguza usalama”, amefafanua Jaji Kibella.
Kwa
upande wake Mtendaji wa Mahakama hiyo Bwana Ernest Masanja, amemueleza Prof.
Mbarawa kuwa kukamilka kwa jengo la Mahakama hiyo kumewezesha Majaji na
watendaji wengine wa mahakama kufanya kazi kwa bidii, ufanisi na kwa wakati
katika kuwapatia wananchi haki.
Katika
hatua nyingine, Prof. Mbarawa ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa
ujenzi wa Hospitali ya Mkoa huo unaosimamiwa na TBA na ameuelekeza Wakala huo
kushirikiana na Mamlaka husika kuhakikisha kuwa ujenzi wake unazingatia viwango
na ubora na kukamilika kwa wakati.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua
jambo kwa viongozi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara alipokutana nao mkoani
humo kwa ziara ya kikazi.
No comments :
Post a Comment