Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA ndugu Alphonce Malibiche akipokea tuzo toka kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli
wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya
Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni. NIDA ilikuwa mshindi wa kwanza
katika kundi la banda bora kwa Wizara na Taasisi za Serikali.
Baadhi ya Watumishi wa NIDA
walioshiriki kufanikisha Maonyesho hayo wakiwa na nyuso za furaha baada
ya kupokea Tuzo ya ushindi. Kutoka kulia ni Edna Wanna, akifuatiwa na
Agnes Gerrald, Raymondn Sengate na Sarah Mashalla.
Katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano na mratibu wa Banda la Maonyesho la NIDA akiwa
ameshikiliwa Tuzo ya Ushindi pamoja na Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu
Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho (kushoto) na kulia ni Ndugu
Jamal Kaoneka wa Idara ya Uhamiaji wadau wakuu wa NIDA katika
kufanikisha Usajili wa Vitambulisho.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
mtendaji wa TRL ndugu Masanja Kadogosa akiwa kwenye picha ya pamoja na
maafisa wa NIDA baada ya kutembelea Banda la NIDA na kuwapongeza kwa
ushindi wa kishindo. Wengine katika picha kushoto ni ndugu Gideon Ndalu
Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama NIDA na katikati ni Ndugu Alphonce
Malibiche Kaimu Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho.
Wananchi wakipata huduma kwenye
banda la NIDA, ambapo huduma ya Usajili na Utambuzi inatolewa, kuchukua
alama za kibaiolijia pamoja na utoaji Vitambulisho kwa wale watakaokidhi
vigezo.
Wananchi wakijaza fomu za maombi
ya Vitambulisho vya Taifa na huduma kwenye Banda la NIDA wakati wa
maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Sabasaba.
………………………………….
Mamlaka ya Vitambusho vya Taifa
(NIDA) imekuwa moja ya Taasisi zilizofanya vizuri katika maonyesho ya
Sabasaba mwaka huu kwa kupata tuzo ya Banda Bora katika kundi la Wizara
za Serikali na Taasisi “Best Exhibitor Government Ministries &
Agencies” kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 41 Sabasaba, yanayoendelea
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa
Dar-es-salaam. Takribani kampuni za Ndani 2500 zikiwemo Wizara na
Taasisi za Serikali zinashiriki maonyesho hayo, pamoja na kampuni za
kigeni 500 zinazowakilisha Nchi 30 duniani.
Maonyesho hayo yaliyoanza Tarehe
28 June 2017 yanatazamiwa kumalizika Julai 13, 2017. Mamlaka ya
Vitambulisho (NIDA) katika maonyesho ya mwaka huu imekuwa ikitoa huduma
mbalimbali kwa wananchi zinazohusu Utambuzi na Usajili wa Watu ikiwemo
huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa na uchukuaji alama za
Kibailojia, kusaidia wananchi waliokwisha sajiliwa na hawajapata
vitambulisho vyao, kujua hatua za Maombi yao pamoja na kutoa Elimu kwa
umma kuhusu faida, umuhimu na matumizi mapana ya Kitambusho cha Taifa
katika ukuzaji Biashara na maendeleo ya Viwanda sambamba na kauli mbiu
ya Maonyesho hayo “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda.
NIDA imehakikisha ushiriki wao
katika Maadhimisho ya mwaka huu unaendana na kasi ya Serikali ya Awamu
ya Tano ya “Hapa Kazi Tu” kwa kuhakikisha wananchi wanaosajiliwa katika
siku 13 za maonyesho hayo wanapata Vitambulisho vyao ndani ya siku hizo.
No comments :
Post a Comment