Saturday, July 8, 2017

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) PROF. MOHAMED JANABI ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA


jana1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
jana2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza viongozi mbalimbali waliotembelea viwanja vya  maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi Taasisi yake inavyofanya kazi za kutibu magonjwa ya Moyo na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka.
jana3
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi wakati alipotembelea  maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
jana4
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Aika Nnkya akimsikiliza Haubert Makoke  ambaye alimuuliza swali kuhusu magonjwa ya Moyo wakati alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri  na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
jana5
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpa ushauri kuhusu afya ya Moyo Mzee John Lihame aliyembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
jana6
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiwaonyesha wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo  lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi upasuaji wa Moyo unavyofanyika.
jana7
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akijibu maswali mbalimbali kuhusu magonjwa ya moyo aliyoulizwa na wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wananchi hao walifika katika banda hilo  kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
jana8
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Fatuma Mkomwa akimpima mapigo ya moyo (BP) Mzee Mwanga  ambaye alifika katika banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ally Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali wanazozitoa.
jana9
Neema Juma akimsikiliza kwa makini Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Pedro Pallangyo wakati akimweleza namna anavyoweza kuishi na kuepukana na magonjwa ya moyo. Neema  alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
jana10
Wananchi wakiwa katika mstari wa  kupima magonjwa ya Moyo bure na kupata  ushauri   katika banda  la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
jana11
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tan trade Edwin Rutageruka (kulia) na  Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi (katikati)   alipotembelea  maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI

No comments :

Post a Comment