Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota,
mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Winnie Kitazi, na kulia ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, SSP Mohamed Kitia.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza na
Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kondoa na Chemba mkoani Dodoma.
Masauni amefanya ziara ya kikazi katika wilaya hizo. Wa kwanza kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na wapili kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Chemba, Simoni Odunga.Wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi wilayani humo,SSP Mohamed Kitia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati)
akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota
wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye
yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati)
akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma, Simon
Odunga,wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo
ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati)
akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kondoa, SSP Mohamed Kitia
wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Ulinzi na Usalama wilayani humo.
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na Mkuu wa Wilaya ya
Chemba, Simon Odunga. Masauni yupo ziara ya kikazi katika Wilaya hizo
ambapo alizitembelea Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akiwasalimia Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kondoa
na Chemba mara baada ya kuwasili mjini Mkondoa kwa ajili ya ziara ya
kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment