Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya
Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya
Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.
Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilzia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS |
Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea
fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa
PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Habari na
Picha wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus, akiweka dole gumba
kwenye fomu ya kujiunga na uanachama wa PSPF kupitia PSS, leo Julai 8,
2017
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa
uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida
kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.
Waziri aliyasema hayo leo Julai 8,
2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na
Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba wakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar
es Salaam yanayoendelea.
“Mimi nitoe wito kwa wananchi
kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi
muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe.
Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi
yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.
“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.
“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.
Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe.
Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari,
kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya
shambani na ufugaji.
“ Hawa wote wanawezakuingia kwenye
mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe.
Waziri.
Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF
Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa za PSPF alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
Baada ya Mwanachi huyu kuelewa huduma
za PSPF na faida zake kwake, hatimaye alikata shauri la kujiunga na
Mpango wa PSS, kwa kujaza fomu kama picha hii inavyojieleza.
Waziri Dkt. Philip Mpango, (kulia),
akipokea mkoba wenye vipeperushi vya taarifa mbalimbali za PSPF, kutoka
kwa balozi wa Mfuko huo, Msanii maarufu Mrisho Mpoto baada ya kutembelea
banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliofika kutembelea banda la Mfuko huo
Bw.Noah Amri, (kulia), Afisa wa Mpango
wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akizungumza na
mwanchi huyu aliyeshika fomu yakujiunga na Mpango huo
Maafisa wa PSPF wakiwa kazini.
No comments :
Post a Comment