Meneja wa mpango wa uchangiaji wa
Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia),
akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji
wa hiari, Mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu (TIA), Bi.Demetriz Bayona,
baada ya kujiunga na Mfuko huo leo Julai 2, 2017. Wananchi wengi
waliotembelea banda la Mfuko huo leo, wamejiunga na mpango huo baada ya
kupatiwa elimu na faida ambazo mwanachama anapata endapo atajiunga na
mpango wa uchangiaji wa hiari ambapo kujiunga hakuna masharti isipokuwa
kwa mtu yeyote mwenye kazi ya kumuingizia kipato na atatakiwa kuchangia
au kuweka akiba ya kima cha chini cha shilingi elfu 10 kila mwezi.
Miongoni mwa faifa ambazo mwanachama aliyejiunga na mpango huo ni pamoja
na kujipatia bima ya afya, itakayomuwezesha kupata matibabu yeye
mwanachama na wategemezi wake watatu. Lakini pia kujipatia mafao
mablimbali yakiwemo fao la elimu, lakini pia mkopo wa nyumba na viwanja
kutegemea na akiba ambayo mwanachama amejiwekea.
Wanachama wapya wa PSPF wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
Bi Amina Mtoo akijaza fomu za kujiunga
na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji
wa hiari, (PSS), leo Julai 2, 2017
Mwanachuo wa chuo cha Uhasibu jijini
Dar es Salaam, Bi.Demetria Bayona, akisikiliza kwa makini faida za
kujiunga na PSPF kupitia mpango wa PSS kutoka kwa afisa wa Mfuko huo.
Baada ya kuelewa faida zake, Mwanachuo huyo hatimaye alijiunga na
kupatiwa kadi yake ya uanachama ndani ya dakika 20.
Menenja wa Mpango wa uchangiaji wa
hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Semba, (kulia),
akitoa somo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko huo kwenye
maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 2,
2017
Meneja Usimamizi wa na utawala wa
mifumo ya TEHAMA, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Bernard Ntelya,
(kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la PSPF
Julai 2, 2017
Afisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), (kulia), akifuatilia jinsi maafisa
wa PSPF wanavyotoa huduma kwa wanachama na wananchi wanaotembela banda
la Mfuko huo. SSRA imeweka maafisa wake kila banda la linalotoa huduma
ya hifadhi ya Jamii ili kusikiliza malalamiko ya wanachama husika wa
Mfuko hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akikaribishwa na Afisa Uhusiano wa
Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Coletha Mnyamani alipotembelea banda hilo
leo Julai 2, 2017.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni
wa PSPF, Bw. Isack Kimaro, (kulia), akimuhudumia mwananchi huyu
aliyefika kupata huduma kwenye banda la Mfuko huo leo Julai 2, 2017.
Afisa wa PSPF, (kushoto), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kupata huduma za Mfuko huo
Bw. Kimaro (kulia), akimsaidia kutambua michango yake mwanachama huyu aliyefika kwenye banda la PSPF
Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni
wa PSPF anayeshughulikia masuala ya uchangiaji wa hiari (PSS), Bi.
Asmahan H. Haji, akiwajibika ipasavyo kwenye dawati lake
Bi Asmahan (kulia), akimkabidhi kadi ya
uanachama wa PSPF kupitia mpango wa PSS, Bi.Amina Mtoo, ambaye
alisindikizwa na mchumba wake, Bw. Ayoub Issa, leo Julai 2, 2017
Afisa Uhusiano wa PSPF, Bi. Coletha
Mnyamani, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, Bi. Gloria P.
Nyange, akiwa na mwanae wa miaka minne Winprecious Noel baada ya
kujiunga na PSS.
Bi Mnyamani akimkabidhi kadi na nyaraka
mbalimbali zinazoelezea jinsi mwanachama huyu mpya Bw.Kamaga Salim
Kilolo, aliyejiunga na mpango wa uchagiaji wa hiari PSS.
Mwananchi akijaza fomu chini ya usaidizi wa Afisa uendeshaji msaidizi wa PSPF
Bi Asmahan H. Haji, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, Bi.Sabah A. Dossa, baada ya kujiunga na mpango wa PSS.
Kabla ya kujiunga na mpango wa PSS, Bi.
Amina Mtoo, (wakwanza kushoto) na mchumba wake, Bw. Ayoub Issa,
walipata fursa ya kupewa elimu ya kina juu ya kujiunga na mpango huo na
faida ambazo mwanachama atapata ikiwemo bima ya afya ambayo itawahusu
wawili hao na wategemezi wao wawili
Bi. Mnyamani akimuhudumia mstaafu
No comments :
Post a Comment