
Meneja Mikopo wa Benki ya Posta
Tanzania, (TPB), Bi.Joanitha Deogratius (kulia), akimuhudumia askari
polisi, Felista Elais, aliyefika kufungua akaunti kwenye banda la Benki
hiyo, jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, viwanja vya Mwalimu Nyerere
maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai
5, 2017 ambako maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam
yanaendelea. Mamia ya wananchi wamejitokeza kufungua akaunti TPB ambapo
kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mikopo wa benki hiyo, alisema wananchi
wanakaribishwa kukopa kwenye benki hiyo ilimradi wakiwa wamejiunga
kwenye vikundi, lakini pia kwa wale wanaotarajia kustaafu, wanaalikwa
kuomba mikopo TPB, ambapo Mkurugenzi wa Mikopo, benki hiyo, Bw. Henry
Bwogi alisema, benki imeanzisha mikopo maalum kwa wataafu. "TPB kwa
kushirikiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ya PSPF, PPF, NSSF, ZSSF,
LAPF na HAZINA inatoa mikopo maalum ili kuwawezesha wastaafu waweze
kukidhi mahitaji yao kwa wakati wanaohitaji." Alisema. Bw. Bwogi.
Alisema wenye sifa za kupata mikopo hii ni pamoja na wastaafu
wanaopitishia pensheni zao kutoka kwenye taasisi za Mifuko ya Pensehni,
ambapo utaratibu wa makato ya marejesho utakuwa umewekwa baina ya Benki
ya Posta na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wastaafu wa wizara ya Fedha.
(NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
Mkurugenzi wa Mikopo wa TPB, Bw. Henry
Bwogi, (kulia), akizunuzma na Waandishi wa habari kwenye banda la benki
hiyo leo Julai 5, 2017
Afisa wa polisi akimsikilzia kwa makini
meneja mikopo wa TPB, Bi.Joanitha Deogratius kuhusu utaratibu wa
kufungua akaunti na kupata mkopo
Baada ya kuelewa utaratibu wa kufungua
akaunti na upatikanaji wa mikopo, sasa ni nyuso za tabasamu na furaha
kati ya Bi. Joanitha(kulia) na Afisa wa polisi Felista.
Afisa w aTPB, Bw.Godbright Mlay, akiwa kazini kwenye banda la TPB.
Mteja wa TPB, akipatiwa huduma za
kibenki kwenye banda la TPB Leo Julai 5, 2017. Kulia ni Mtoa huduma
(Teller), Bi, Shufaa Mohammed.
Meneja mikopo wa TPB, Bi. Joatha
Deogratius (kushoto) na Afisa Mauzo wa benki hiyo, Bi.Heavelight Uisso,
(wapili kushoto), wakiwahudumia wateja hawa waliofika wkenye banda la
TPB leo Julai 5, 2017.
Kikosi kazi cha TPB kikiongozwa na Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa benki hiyo, Bi. Chichi Banda, (wapili kulia),
kilichoko kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam.







No comments :
Post a Comment