Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato Bi.
Winfrida Lawrent(65) kutoka Kata ya Kasenga kabla ya kuwakabidhi msaada
wa vyakula mbalimbali ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga
wa mahindi, Kilo 4000 Maharage, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato Bw.
AnatoryBisate (64) kabla ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali
ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga wa mahindi, Maharage
kilo 4000, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akiwakabidhi kwa pamoja mafuta waakilishi wa Wazee kutoka kata ya
Kasenga AnatoryBisate (64) kulia pamoja na Bi. Winfrida Lawrent(65)
kushoto mara baada ya kuzungumza na wazee 400 katika Ukumbi wa
Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akiimba pamoja na wanakwaya wa Mwagazege mara baada ya kuwasili katika
ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mama Janeth Magufuli akiwasili
katika eneo la mkutano mara baada ya kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita
Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga Chato mkoani Geita.
Mama Janeth Magufuli akiwa na
viongozi wengine wa mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali
Mstaafu Ezekiel Kyunga wakwanza kushoto wakati wa dua kabla ya
kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi ya 400.
Mama Janeth Magufuli akifurahi
pamoja Naibu Waziri wa nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wakati
Kwaya ya Mwakazege ya kutoka Chato ilipokuwa ikitumbuiza kabla ya
kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi ya 400.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akizungumza na Wazee wasiojiweza zaidi ya 400 kutoka Wilaya ya Chato
katika Ukumbi wa Mshikamano Saccos.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa, Wilaya na
Chama waliojumuika na Waakilishi wa wazee wasiojiweza zaidi ya 400 Chato
mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
Wazee wakishangilia wakati wa hotuba ya mgeni rasmi.
PICHA NA IKULU
No comments :
Post a Comment