Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni katika katika banda
la Mahakama sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Aliyesimama mwenye
miwani ni Jaji wa Mahakama Kuu
Mhe. Edson Mkasimongwa.
Mhe. Edson Mkasimongwa.
………………….
Na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania.
5/07/2017
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, amesema
kwamba Mahakama ya Tanzania imejipanga kusikiliza kesi zilizokwama
zinazohusu mabenki kwamba ili ziweze kwenda kwa haraka na
kulingana na sera ya, ikiwemo kuwezesha
ukuzaji wa uchumi wa nchi .
Kauli
hiyo ilitolewa na jana Kaimu Jaji Mkuu huyo , wakati alipotembelea
Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba yanayoendelea
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko,
Barabara ya Kilwa Road jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumzia kuhusu
mlundikano wa kesi mahakamani alisema Mahakama ya Tanzania inafanya
mikakati ya kuweza kuzipunguza.
“ Tunahitaji majaji zaidi ya 30 ili kuweza kupunguza mlundikano uliopo wa kesi zilizopo Mahakamani,” alisema Profesa .
Profesa
Juma alisema hayo, baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya
maonesho, ambapo alisema Mahakama ya Tanzania, imepiga hatua katika
mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), akitolea
mfano Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara, ambapo
alishauri kwamba mahakama zingine za chini ziweze kujifunza.
Profesa
Juma pia alitoa ushauri kwa watu wenye viwanda nchini kufuata
sheria na taratibu, waweze kusajiliwa kwa kuwa kufanya hivyo
kutawafanya washiriki kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi wa nchi .
“
Nimetembelea Banda la Mkemia Mkuu wa Serikali nimeona mazao na
bidhaa mbalimbali,hivyo ni vema watu wanaotengeneza bidhaa
wakasajiliwa ili waweze kufuata sheria na taratibu za nchi, kwa kuwa
kufanya hivyo kutawezesha bidhaa zao kuwa bora na wataweza kuiwezesha
nchi kushiriki katika uchumi wa kisasa,” alisema Profesa Juma.
Katika
maonesho hayo, Kaimu Jaji Mkuu huyo, miongoni mwa mabanda
aliyoyatembelea banda la Mahakama ya Tanzania, Jeshi la Magereza ,
Banda la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam(UDSM),banda la Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikal(GCLA)i,
banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA). Banda la Wakala wa
Usajili , Ufilisi na Udhamini (RITA) Mamlaka ya Reli Tanzania, na
Mabanda la Mamlaka ya Reli Tanzania, Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)
,Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC .
No comments :
Post a Comment