Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo
wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20
walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo
katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya
Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa
Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za
taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti
la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook
pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza
wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka
mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele
cha Uhuru .
Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa
mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza
mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka
usawa wa bahari .
Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya
mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani
(FIFA) ,Jonesia Rukyaa kuchezesha mchezo huo wa dakika 90 uliomalizika
kwa sare ya bila kufungana .
No comments :
Post a Comment