Friday, June 30, 2017

MAMIA WAFURIKA ILI KUJIPATIA VITAMBULISHO VYA TAIFA KATIKA BANDA LA NIDA VIWANJA VYA SABASABA

1
Bi. Rose Mdami Mkuu wa Kitengo cha Mawasiiano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA akiwahudumia wateja mbalimbali waliofika katika banda la Mamlaka hiyo ili kupata huduma ya kupatiwa vitambulisho vya taifa katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
2 3
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wakitoa huduma kwa wananchi mbalimbali waliofika katika banda hilo ili kupatiwa vitambulisho vya taifa leo.
4
Wananchi mbalimbali wakiwa wamefurika kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa NIDA katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
5
Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakiendelea na kutoa huduma katika banda hilo.

No comments :

Post a Comment