NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
SIKU
moja kabla ya pambano la fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2017,
almaarufu kama UEFA Champions League, kocha mkuu wa Real Madrid, Mfaransa,
Zinedine Zidane, alimwagia sifa lukuki Mshambuliaji wake kutoka Ureno, Christiano
Ronaldo, kuwa anajua kulisakata kabumbu pengine kuliko yeye (Zidane) wakati
akicheza na kwamba anaamini Ronaldo ataiongoza vema safu ya ushambuliaji ya
timu hiyo kuibuka mshindi na kutwaa kombe hilo dhidi ya Juventus ya Italia,
usiku wa kuamkia leo Juni 4, 2017 mjini Cardiff, Wales..
Ama
kwa hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa, Christiano Ronaldo, akipachika mabao
mawili,Casemiro bao moja na Marco Asenso bao moja na hivyo Madrid kuibuka na
ushindi mnono wa mabao 4-1, bao la Juventus lilipachikwa wavuni na Mandsukic,
ambaye alifunga bao zuri la ksuawazisha.
Ushidni
huo unaifanya Madrid, kuwa timu ya kwanza barani Ulaya kufanikiwa kulitete taji
lake la mabingwa Ulaya na Juventus kwa mara ya kwanza inakubali kipigo kikubwa
cha mabao katika mchezo wa fainali katika historia yake.
Hata hivyo mshambualiaji wa Juventus,
alilambwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya njano mara mbili kwa
kumchezea vibaya tena kwa makusudi, mlinzi Sergio Ramos na hivyo
kuwalazimu kucheza pungufu uwanjano japo kwa dakika chache za kipindi
cha lala salama.
No comments :
Post a Comment