Friday, June 30, 2017

IGP SIRRO AWATIA MOYO WANAKIJIJI WA MICHUKWI, WILAYANI KIBITI MKOANI PWANI KUFUATIA MAUAJI YA VIONGOZI WAO

3


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti Juni 29, 2017 alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji  hayo.(PICHA NA HASSAN MNDEME WA JESHI LA POLISI)

unnamed
IGP Sirro akisalimiana na wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji.

1
Mkuu wa Meshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti mkoani Pwani Juni 29, 2017 alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji hicho. IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo na kuwataka kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.


2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji hicho

No comments :

Post a Comment