Makamu
wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji,
akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, ambaye amemwakilisha Rais John
Pombe Magufuli.
#BMGHabari
Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe
(kulia), akizindua “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka
2016”. Kushoto ni mjumbe bodi ya Misa Tanzania, Lilian Lucas.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe,
akizindua “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016”.
Uzinduzi wa “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016”.
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo
amezindua “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa
mwaka 2016” kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.
Akizungumza
mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na
kulinda uhuru wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za
uchunguzi huku akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za
uchunguzi badala ya habari za kihisia.
Afisa
Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika
(MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba
taarifa hiyo imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari
Mosi hadi Disemba 31, 2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama
wa SADC.
No comments :
Post a Comment