Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory
Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha
ardhi kinyume cha sheria
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) wakihakiki nyaraka na
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kulia) katika ziara ya Mhe.
Lukuvi mkoani Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.
Godfrey Zambi, watendaji na viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika
mkutano wakati wa ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango Miji
na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza kuhusu utaratibu za upangaji
mijina umilikishaji ardhi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa
Mipango Miji wa Lindi akijieleza kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na na
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi katika ziara ya Mhe. Lukuvi
mkoani Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mafaili katika masijala
ya ardhi mkoani Lindi ambapo alibaini mapungufu ya kutokuwa na usahihi
wa uwekaji kumbukumbu za ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.
Godfrey Zambi wakikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi
mkoani Lindi
Ndugu Gibson Mwaigomole Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Lindi.
………………..
|
Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Afisa
Mipango Miji wa Lindi Ndugu Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya
ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kumilikisha kampuni
ya
Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.
Mhe. Lukuvi aligundua hayo baada
ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa na badala yake
kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa
kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo
kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais.
Aidha, Afisa Mipango Miji huyo
aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada
ya kuandika barua na kuisaini kwa niaba ya Afisa ardhi wakati yeye ni
Afisa Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate
ambalo pia ni kosa kisheria.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu
Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate
Senje amesema kwamba utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa
ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na
baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wana kijiji.
“Kama nyie hamna uwezo wa
kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kazi kuanzia leo hafai kuwa
mtumishi wa serkali” alisema Mhe. Lukuvi na kuagiza eneo hilo lirudi na
kuwa mali ya serikali “ Sasa hiyo ardhi lazima irudi itakua mali ya
serikali kuanzia leo” .
katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi
ametembelea ofisi za ardhi Lindi na kufanya ukaguzi katika Masijala za
ardhi na kuangalia mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, kisha
kuwaagiza watendaji wa ardhi mkoani hapo kuhakikisha wanatoa hati kwa
wakati na kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa kila mmiliki wa ardhi ili
kuongeza pato la serikali.
Pia alitembelea ofisi za Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani hapo na kupokea taarifa kutoka kwa
Meneja wa shirika hilo mkoani Lindi Ndugu Gibson Mwaigomole. Katika
taarifa hiyo Mhe. Lukuvi amelishauri Shirika la Nyumba la Taifa kufanya
uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za kisasa pamoja na Nyumba
zenye gharama nafuu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.
Godfrey Zambi akiwa pamoja na waziri Lukuvi na watendaji wa mkoa
ameeleza kuwa sekta ya ardhi mkoani hapo inachangamoto nyingi lakini
ofisi yake inaendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha
changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa maslahi ya watu wa
Lindi na Tanzania kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment